- Kilimo

Otesha miti kwa manufaa yako na kizazi kijacho

Sambaza chapisho hili

Wanajamii wengi hawatambui umuhimu wa miti katika kilimo, mazingira, kwa binadamu na hata kwa wanyama jambo ambalo wengi wamelipuuzia na kutokulichukulia maanani.

 

Tunapozungumzia miti, kwa ujumla tunamaanisha miti ya asili ambayo zipo katika misitu yetu na hata maeneo yetu ya makazi pamoja na ile ya kuotesha inayotupatia rutuba ya udongo, hewa safi, chakula cha wanyama, kivuli, mbao, kuni, madawa pamoja na matunda ya aina mbalimbali.

Faida za miti

Kuna faida nyingi sana za miti lakini zifuatazo ni baadhi tu ya faida;

  • Miti hutupatia hewa safi ya oksijeni ambayo binadamu na wanyama hutumia katika kuishi.
  • Miti husaidia kusafisha hewa pamoja na kupunguza joto la hewa.
  • Miti husaidia kupunguza hasara zisababishwazo na upepo lakini wakati wa joto miti huleta kivuli na kupunguza kazi ya joto katika mazingira yetu.
  • Miti husaidia kupunguza mmomonyoko wa udongo, kupunguza athari za mafuriko yanayotokana na maji ya mvua lakini pia husaidia kuhifadhi maji ya mvua.
  • Miti pia huongeza thamani ya nyumba ikiwa ni miongoni mwa mali zisizohamishika hawa wakati wa uuzaji wa maeneo au upanuzi wa shughuli mbalimbali za nchi.
  • Miti hutupatia matunda mbalimbali ambayo hutumika kama chakula au kiburudisho na kujenga afya ya binadamu.
  • Miti hutupatia chakula cha wanyama kwani kuna baadhi ya miti majani yake hutumika kulishia mifugo.
  • Miti hutupatia kuni, mkaa na ni moja ya kitega uchumi cha kibiashara hasa katika ujenzi kwani hutupatia nguzo na mbao.

MUHIMU: Katika msimu huu wa mvua ni vyema sana kwa wanajamii kuotesha miti ya aina mbalimbali ili kuhakikisha faida tajwa zinapatikana katika jamii.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *