Ngozi hukaushwa ili kuzuia uharibifu unaotokana na kuoza kwa kuwa si ngozi zote zinazozalishwa hupelekwa kiwandani zikiwa mbichi ili kusindikwa.
Ngozi zikioza hupoteza ubora wake na hivyo kutokuwa na manufaa katika matumizi mbalimbali. Ngozi ni zao la mifugo linaloweza kutoa mchango mkubwa kuwainua kiuchumi wafugaji na jamii kwa ujumla.
Baadhi ya wajasiriamali hutengeneza bidhaa mbalimbali kutokana na ngozi ya ng’ombe, mbuzi na kondoo.
Hata hivyo, shughuli ya uzalishaji imekua na changamoto ikiwemo ubora hafifu wa bidhaa na makusanyo madogo ya ngozi kutokana na ufugaji usiozingatia kanuni bora za ufugaji. Katika toleo lijalo, Mkulima Mbunifu itakuletea makala ya usindikaji wa ngozi baada ya kuchunwa.
Maoni kupitia Facebook