Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mabadiliko makubwa katika kilimo na mbinu za uzalishaji. Utafiti umeonyesha kuwa mbinu asilia za kilimo hai zina faida zaidi kuliko zile zinazojumuisha kemikali au vitu vingine hatari.
Siku hizi, bidhaa za kilimo hai zinapatikana kwa urahisi katika maeneo mengi. Hii inamaanisha kuwa kuna ushindani kati ya wazalishaji wa kilimo hai. Ikiwa unataka kufanikiwa katika soko, utalazimika kuwashirikisha watumiaji kutoka mwanzo wa biashara yako.
Hii si kazi rahisi. Kama mkulima, unaweza kukabiliwa na changamoto kadhaa kwenye njia yako ya kufikia ama kujenga soko kubwa. Kuna wauzaji wengi wanaojitokeza, hivyo, lazima uonekane wazi ili kuvutia wateja. Ingawa, mwishowe, yote yatategemea ubora wa bidhaa au mazao yako, hata hivyo, jinsi unavyouza bidhaa pia ni muhimu sana.
Kimsingi, haijalishi mazao yako ni mazuri kiasi gani, unahitaji kuitangaza vyema ili kuvutia macho ya mteja wako. Vinginevyo, hakuna kitu kitakachofanya tofauti, iwe ni vifungashio, vile unavyofunga bidhaa, nembo na mambo mengine. Hapa tunakueleza mikakati michache ambayo inaweza kukusaidia kupata na kujenga soko la bidhaa yako za kilimo hai.
Tambua soko unalolenga
Kabla ya kuingia katika juhudi za uuzaji, ni muhimu kujua wateja wako ni akina nani. Bainisha idadi na mahitaji yao ili kujua kiasi ya uzalishaji utakayofanya. Kwa mfano, je ni watu wanaojali afya zao, watumiaji wanaojali mazingira, au wanapenda vyakula vinavozalishwa katika eneo lako? Kuelewa soko unalolenga kutakusaidia kujua vile utakavyotangaza bidhaa na kufikia watu wanaofaa.
Uzalishaji thabiti
Ni lazima upange na kuzalisha kila wakati bila kukosa. Ikiwa kwa sababu yoyote ile ambayo iko nje ya uwezo wako huwezi kuleta mazao yako sokoni basi kuwa na chanzo mbadala cha mazao kwa wateja wako. Unaweza kuwaelekeza kwa mkulima mwingine au ukanunua mazao kutoka kwa mkulima mwenyewe. Ingawa hakuna uhakika kwamba wateja wako watarudi kwako mara utakaporejelea uzalishaji na kuleta mazao yako sokoni,Unaweza kuwapoteza!
Pia, hakikisha kuwa mazao yoyote unayonunua kutoka kwa wakulima wengine na kuwaletea wateja wako yanafikia ubora ambao wamezoea kupata kutoka kwako. Ili kuzalisha nyakati zote, kusanya na hifadhi maji kwa matumizi ya baadaye, hasa msimu wa kiangazi. Kufuatana na hili, unaweza kutumia teknolojia ya umwagiliaji maji kwa matone ili maji hayo yaweze kutumika kwa muda mrefu, mpaka mvua inyeshe tena.
Uza kwa majirani
Kwa kawaida, soko la kwanza kwa mkulima mdogo wa kilimo hai ni majirani na jamii iliyo karibu. Unaweza kushangazwa sana na kiasi cha mauzo utakayofanya kutoka kwa majirani, marafiki na jamii inayokuzunguka. Kuna msemo kwamba kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza, hivyo, mteja mmoja aliyeridhika atakuletea mteja mwingine kwako. Kwa hivyo, kuwa thabiti katika kutangaza bidhaa zako. Waambie jinsi mazao yako yalivyo mazuri. Wakati huo huo, kuwa na uhusiano mzuri na wateja.
Shirikiana na mgahawa iliyo karibu
Mgahawa iliyo karibu au hata ya mbali ni soko nzuri na ya kutegemewa ya mazao na bidhaa yako. Mbali na kununua moja kwa moja kutoka kwako, pia unaweza kutumia njia
hii kutangaza mazao yako na kuwafikia wateja wengine. Wateja wao wanaporidhika na hali ya juu ya chakula kinapikwa kutokana na mazao yako na kupata manufaa, mazao yako yanaaminika na yenye afya. Hii ni njia moja ya kutangaza bidhaa.
Shirikiana na wateja
Watu kadhaa huwa na tabia ya kupata viungo na mazao kutoka kwa maduka ya bidhaa kwenye soko la wakulima au maduka madogo. Kwa hakika hii ni sehemu muhimu ya ushirikiano na jamii ya wateja kuhusu namna unavyozalisha mazao yako ili yawe yenye afya, safi, salama na ya ubora wa hali ya juu.
Siku hizi, watu wamehamasika. Wengi wao wangependa kujua bidhaa au mazao wanayonunua yametoka wapi. Kwa mfano, kuna mazoea potufu ya baadhi ya wakulima kuzalisha mbogamboga wakitumia maji chafu au kutumia kemikali nyinyi ambayo inaweza kudhuru afya ya walaji. mazoea Unapojumuika, kuongea na kushirikishana na wateja wako, wanapata kujua kwamba bidhaa zako ni za uhakika na hakutakuwa na matatizo yoyote kwa afya zao baada ya matumizi.