Mazao ya mbolea ya kijani ya jamii ya mikunde (ambazo ni zile zinatengeneza mbolea ya naitrojeni kutoka kwenye naitrojeni iliyopo kwenye hewa) zinaweza kuwapa wakulima wadogo faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na:
- Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni kwa ajili ya udongo.
- Zinaongeza tani nyingi za viumbe hai kwenye udongo, hivyo basi, kuongeza udongo wenye rutuba, uwezo wa kutunza maji, kiasi cha virutubisho, uwezo wa kuvunjikavunjika na muundo wa udongo.
- Mazao ya mbolea ya kijani yanapelekea kwa urahisi usafirishaji wa virutubisho kwa mimea.
- Mazao ya mbolea ya kijani hayana gharama zaidi ya manunuzi ya mbegu.
- Mazao ya mbolea ya kijani zinatoa kivuli kwenye udongo mpaka miezi kumi na moja kwa mwaka, sababu ambayo ni ya muhimu zaidi katika nchi zenye hali ya hewa kwa ajili ya utunzaji wamaji kwenye udongo na viumbe hai.
- Kivuli kinachotokana na hii mimea inazuia udongo kutopotea kwa njia ya upepo na maji.
- Mazao ya mbolea ya kijani yanapelekea kupatikana kwa malisho yenye wingi wa protini kwa wanyama na ni muhimu zaidi yanapopatikana katika kipindi cha miezi ya mwisho ya kiangazi (kama vile malisho katika kipindi cha mwaka huu ni kikwazo kwa ufugaji wa wanyama kwa njia za kienyeji).
- Baadhi ya mazao ya mbolea ya kijani ni chakula cha binadamu, hasa maharage ya kuliwa, njegere na mbegu.
- Mazao ya mbolea ya kijani yanaweza kutoa kipato kwa kuuza kuni, chakula au malisho (labda na mbegu).
- Yanasaidia watu kuacha njia hatari za kienyeji, kama vile kuchoma mabaki ya mazao au kuachilia wanyama kipindi cha kiangazi na kula kila kinachoonekana.
- Baadhi ya mbolea ya kijani yakichanganywa na nafaka za msingi, zinaweza kuzuia magugu hivyo basi kuzuia gharama za uendeshaji wa kupalilia.
Mlinganisho wa mbolea
Kutokana na kwamba utengenezaji wa mbolea ni teknolojia ambayo inashauriwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika nchi za dunia ya tatu, itakua ni vizuri kulinganisha utengenezaji wa mbolea na matumizi ya mazao ya mbolea ya kijani.
- Mbolea haiozeshi tu vitu vilivyotokana na viumbe hai ambayo tayari inayo, ilhali mbolea ya kijani yanaweza yakaongeza zaidi ya tani arobaini ya vitu vitokanavyo na viumbe hai kwa hekari moja. Vitu vitokanavyo na viumbe hai mara nyingi huwa ni kwa kiasi kidogo katika mashamba ya wakulima (au tayari imekwisha kutumiwa tena)
- Zaidi ya yote, mbolea itarejesha takriban asilimia 98 ya naitrojen katika shamba lakini mazao ya mbolea ya kijani, yataongeza kiasi chote kinachotakiwa cha naitrojen mpya katika mfumo.
- Mkusanyiko wa mbolea huitaji maji. Hii ina maanisha kwamba inaandaliwa sehemu iliyo karibu na vyanzo vya maji lakini katika umbali kidogo na pale inapotengenezwa.
Mazao ya mbolea ya kijani yanapandwa ili kusaidia maji ya mvua kutumika kwa vitu vingine lakini pia hupandwa katika eneo ambapo yanahitajika na yatatumiwa.
- Mbolea haiwezi kutumika kama chanzo cha chakula iwe ni kwa wanyama au kwa binadamu lakini mbolea ya kijani hutumika kama chakula kwa wanyama na hata kwa binadamu.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Charles Bonaventure kwa simu namba 0717343723 cbonaventure@echonet.org