- Kilimo

Kua mlemavu isiwe kikwazo cha kutofanya maendeleo

Sambaza chapisho hili

Kumekua na dhana katika jamii zetu kuona mlemavu hawezi kufanya jambo lolote la msaada katika jamii yetu. La hasha, watu wenye ulemavu wanauwezo wa kufanya mambo kadhaa iwapo watapatiwa fursa na msaada.

Hata hivyo kuna ulemavu wa aina mbili, ulemavu wa kuzaliwa nao na ulemavu kutokana na ajali katika maisha. Katika makala hii Mkulima Mbunifu inamuangazia mlemavu Bwana Ibrahimu Kajia Mkazi wa Mbale, kijiji cha Mbole, Wilayani Mwanga (Usangi)-Kilimanjaro.  Alipata ulemavu wa kupooza upande wa kulia wakati akirekebisha nyaya za umeme kwenye dari.

Mimi ni mnufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu (MkM), nililiona kwa mara ya kwanza kutoka kwa Bwana Mohamed H. Msangi wa Usangi Interchick. Nilimuomba na kumuuliza hawa watu nitawapataje kwani ningependa pia kupokea jarida hili.

Alikua akijishughulisha na ufundi wa umeme majumbani, baada ya kupata tatizo la kupooza akaamua kujikita kwenye kilimo cha mbogamboga na mke wake pamoja na usindikaji wa bidhaa za maziwa.

Kwasasa Bwana Ibrahim, mjasiriamali mdogo anatengeneza siagi, samli, maziwa ya mgando na ice cream. Bidhaa hizi anaziuza katika soko la mtaani. Jamii jirani inatambua shughuli yake na hivyo hufuata kununua bidhaa hizo kwake.

“Nalipenda jarida la Mkulima Mbunifu kwani nimefanikiwa kwa kujifunza kutoka kwa watu mbalimbali ambao walieleza jinsi wanavyosindika bidhaa mbalimbali za maziwa. Hata hivyo ninaamini nafasi hii itanipa fursa na mimi kujulikana na wasomaji wenzangu ili niweze kupata wateja wengi zaidi.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *