Kanuni za kilimohai zinavyofungamana na mazingira
Kanuni ndio msingi wa kilimo hai na mchango unaoweza kuifanya dunia kuboresha kilimo duniani kwa ujumla. Kilimo ni moja ya shughuli muhimu zinazofanywa na binadamu kwa ajili ya kupata mahitaji ya kila siku ili kujikimu. Historia, mila na tamaduni za watu katika jamii zinaambatana na maendeleo katika kilimo.
Kanuni zinazotumika katika kilimo kwa ujumla zianahusisha mtazamo wa watu juu ya udongo, maji,mimea na wanyama katika kuzalisha, kuandaa na kusambaza chakula na bidhaa nyinginezo.
Shamba la kilimo hai likiwa limelimwa mbogamboga za aina mbalimbali [Picha; SAT]
Kanuni hizo zinaonesha namna watu wanavyo ona uhai na mandhari ya ardhi, mahusiano miongoni mwao na mwelekeo wa matumaini kuhusu vizazi vijavyo. Kanuni za kilimo hai zinalenga kuhuisha vuguvugu la kilimo hicho katika nyanja zote, kutoa mwongozo katika kuweka vipaumbele juu ya maendeleo, mipango na viwango. Isitoshe, kanuni hizi zinawakilisha mtazamo wake kidunia.
Kanuni za msingi wa kilimo hai: Kuna kanuni nne za msingi wa kilimo hai.
- Kanuni ya Mazingira
- Kanuni ya Afya
- Kanuni ya Haki na Usawa
- Kanuni ya Huduma
Kanuni hizi zimefungamana na kwa ujumla wake zinabeba kivitendo matarajio ya kilimo hai japo kila moja ya kanuni ina maelezo yake na dhana iliyobebwa ndani yake huku zikizingatia afya ya mazingira na mimea, Wanyama na binadamu.
Usiache kufuatili makala hii kwa undani katika tolea la Mkulima Mbunifu, toleo la 112 la January 2022