Dawa ya kufukuza wadudu
Dawa hii hutumika kudhibiti wadudu kama nzi weupe katika mipapai, nyanya, tikiti, vitunguu, mboga-mboga na matunda.
Mahitaji muhimu
- Mchele kilo 1
- Maji lita 1
- Chombo cha ujazo wa lita 2.
Jinsi yakutengeneza
Changanya mchele na maji katika chombo kisafi chenye mfuniko wakubana. Vundika kwa siku saba, baada siku saba itakuwa tayari kwa matumizi.
Matumizi
Chukua kiasi cha mils 30mls changanya na maji lita 1 kisha puliza katika mimea yako iliyoadhirika na wadudu Hawa weupe.
NEMSOL -3
Kudhibiti vimamba, ubwiri wa juu na wachini katika mazao ya mboga-mboga, matunda na nafaka.
Mahitaji muhimu
- sabuni ya maji mils 10s
- Mafuta ya mwarobaini mils 10
- Bicarbonate gramu 10
Jinsi yakutengeneza
Changanya malighafi zote hapo juu katika lita moja ya maji na Kisha kuipuliza katika majani yaliyoadhirika. Puliza sehemu za chini na juu ya majani.
Matumizi
Chukua mils 10 na changanya na maji lita 1 kisha puliza kwenye mimea
NEEMSOL-6
Dawa hii limepewa hilo jina kwakuwa Ina viambata vya asili aina sita. Hii kirahisi kukumbusha mahitaji muhimu wakati wakuandaa dawa hii kwakutumia vipimo maalum. Hudhibiti magonjwa na wadudu karibu katika mimea yote kwakuwa ina wigo Mpana. Vimamba, utitiri mwekundu, utitiri mweupe, utando wa buibui, viwavi (caterpillars), ubwiri wa juu, ubwiri wa chini, mnyauko n.k
Mahitaji muhimu
- Ndulele gramu 100
- Majani ya mwarobaini gramu 100
- Mapapai gramu 100
- Sabuni yam aji mils 100
- Pilipili kali gramu 50
- Bicarbonate paketi moja yenye ujazo wa gramu 70
- Maji lita 20
Jinsi yakutengeneza
Twanga- malighafi ngumu katika kinu chako kisha changanya na malighafi laini kwa muda wa masaa 24 Kisha chuja kwa kitambaa safi. Chuja mara mbili hadi tatu.
Matumizi
Chukua mchanganyiko wote katika Lita 20 Kisha puliza kwenye mimea yenye mwezi mmoja au zaidi
Mkojo wa sungura (rabbit urine.
Jinsi yakutengeneza
Vundika mkojo kwa siku saba katika chombo kisafi kisichopitisha hewa au mfuniko wakubana.
Matumizi
Tumia lita 1.5 changanya na lita 15 za maji kisha puliza katika mimea yako kufukuza wadudu. Dawa hii pia wakati huo huo huongeza kiwango ha nitrojeni katika mimea yako.
Mkojo wa sungura
Hutumika Kama dawa yakufukuzia wadudu pia kuongeza nitrojeni katika mmea kwa njia yakuchachusha kwakutumia mollasI
Mahitaji muhimu
- Lita za mkojo 5
- Mollasi Lita 5
Jinsi yakutengeneza
Vundika kwa siku 14. Katika chombo kisichoruhusu hewa kuingia au kutoka.
Matumizi
Tumia 1.5L katika 15 za maji. Dawa hii hukaa bila kuharibika kwa miezi 6
KILUMAGIO
Hii Ni dawa inayodhibiti viwavi jeshi vamizi katika mimea jamii ya nafaka. Kama mahindi, mtama n.k
Mahitaji muhimu
- Spidex mils 55
- Sukari kilo 1
- Unga wa mahindi kilo 5
- Maji lita 1
Jinsi yakutengeneza
Changanya malighafi malaini kwanza pembeni Kisha changanya katika malighafi malaini kwa mkono. Hakikisha umevaa gloves wakati unaifanya hii zoezi. Changanya hadi malighafi yote yatakapochanganyika vizuri. Kisha hifadhi sehemu Safi katika mfuko.
Matumizi
Weka kidogo kwakudondosha vipunje vidogo vya dawa katika sehemu ya katikati ya mmea. Anza kuweka baada ya siku 10 hadi 15 toka umepanda mahindi Kisha rudia kila baada ya siku 14. Hukaa mwezi mmoja ikiwa imehifadhiwa (sealed)
Vimi-fly
Hii dawa inatumika kudhibiti utitiri mweupe nzi weupe katika nyanya, papai, tikiti na mazao ya mboga mboga
Mahitaji muhimu
- Lita 25 za maji
- Kilo moja ya unga wa ngano
- Lita tatu na robo ya maziwa
- Siki [vinegar] vijiko viwili vya chai
Jinsi yakutengeneza
Chukua vinegar nyeupe Kisha weka katika kikombe kimoja Cha maziwa. Chukua unga wa ngano kilo moja kicha changanya katika maji Lita 20. Changanya malighafi yote kwa pamoja kisha koroga kwa dakika mbili.
Matumizi
Chuja Mchanganyiko wote kwa kitambaa safi Kisha gawa katika solo yako kwa ajili ya matumizi shambani.
Dawa ya kufukuza wadudu (repellents)
Dawa hii nikwaajili yakufukuza wadudu shambani.
Mahitaji muhimu
- Saumu gramu 10
- Pilipili kali gramu 10
- Sabuni ya maji lita 1/majani ya mpapai
- Maji lita 1.
Jinsi yakutengeneza
Twanga- malighafi magumu pamoja kisha changanya na malighafi malaini. Kisha chuja kwakutumia kitambaa safi.
Matumizi
Chukua mchanganyiko wote katika Lita moja ya maji Kisha puliza kwenye mimea yako kufukuza wadudu. Inashauriwa kupuliza kabla wadudu hawajaingia shambani.
EM5
Hawa ni vimelea wa tija (beneficial microbes). Dawa hii hutumika katika kuondoa vimelea wabaya wanaosababisha magonjwa katika mimea nakuongeza vimelea wazuri katika mimea na udongo
Mahitaji muhimu
- Majani ya mwarobaini gramu 200
- Maua ya bangi pori gramu 100
- Pilipili kali gramu 50
- EMAS mils 200
- Siki [vinegar] mils200
- Spirit/konyagi mils 200
- Maji lita 1.2
Jinsi yakutengeneza
Twanga malighafi magumu katika chombo moja Kisha changanya na malighafi malaini Kisha weka katika ndoo yenye mfuniko wakubana vizuri kwa siku 14. Kisha itakuwa imeiva. Chuja mchanganyiko wako vizuri tayari kwa matumizi.
Matumizi
Chukua mils 10 ya Em5 katika lita 1 ya maji. Kisha changanya na puliza kuondoa vimelea wabaya na kuongeza vimelea wazuri kwenye udongo.