Huu ni msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini. Bila shaka wengi wetu ni wakulima na wafugaji hivyo bado tunaendelea na shughuli zetu za kila siku. Je, ni changamoto zipi unazopitia katika msimu huu wa mvua kwenye shughuli zako za kila siku za kilimo?Tushirikishe/tueleze/Tuulize ili tuweze kupeana ushauri nini chakufanyaTuma ujumbe wako hapahapa au kupitia namba 0762 333 876 au…
Kilimo
VACANCY: TERMS OF REFERENCE FOR MKULIMA MBUNIFU (MKM) INTERNAL EVALUATION CONSULTANT
SAT seeks to recruit a consultant to support MkM project to carry out a rapid progress evaluation for the implementation period running from January 2023 – June 2024. CLICK THE LINK HERE https://mkulimambunifu.org/wp-content/uploads/elementor/20240429_TOR-for-Evaluation-Consultant_1.pdf
Tumia molasi kurejesha rutuba ya udongo
Katika kilimo, matumizi ya Molasi ni muhimu kwa kuboresha hali ya udongo, kudhibiti wadudu, kuwezesha udongo kuwa na rutuba, kurekebisha hali ya udongo na pia kupunguza matatizo kwa mimea inayopandikizwa. Matumizi na kiasi cha kutumia Kuboresha umbile la udongo. Molasi husaidia kuboresha udongo na kuunganisha chembe za udongo na chembe za rutuba na viumbe hai ardhini. Ili kuwa na matokeo…
Mazao ya Chakula yasiyopewa kipaumbele yenye Afya.
Mazao yasiyopewa kipaumbele yenye afya, au “Neglected and Underutilized Crops (NUS),” ni mazao ambayo mara nyingi hupuuzwa au kutotumika ipasavyo licha ya faida zao za lishe na afya. Hizi ni aina za mazao ambayo hayajapata umaarufu au uwekezaji wa kutosha katika kilimo au matumizi ya lishe, ingawa yana thamani kubwa katika kuboresha afya na lishe. Kuna sababu kadhaa zinazochangia mazao…
Namna ya kuongeza rutuba ya udongo
Ongezeko la uhitaji wa chakula duniani kutoka katika eneo lile lile dogo linalotumika kwa uzalishaji, huku ardhi hiyo ikikabiliwa na madhila kama vile mmomonyoko wa ardhi mabadiliko ya tabia nchi na ongezeko la wadudu na magonjwa kumeathiri uzalishaji kwa kiwango kikubwa hivyo kupelekea uboreshaji wa udongo kuwa kipaumbele cha kuzingatia. Viini vya rutuba ya udongo hutoka wapi Rutuba ya…
Tumia mitego kunasa wadudu wkenye matunda na mboga
Kutengeneza mitego mwenyewe Ili kutengeneza mtego wa kunata, sambaza petroleum jeli au oili chafu kwenye mbao laini, iliyopakwa rangi ya njano (ukubwa wa sm 30 kwa sm 30). Weka mitego karibu na mimea lakini ikae mbali kidogo kutoka kwenye shina ili kuzuia majani yanayoanguka yasinase kwenye bodi. Chukua tahadhari kwamba rangi ya njano huvutia aina nyingi za wadudu, wakiwemo wadudu…
Mmea wa artichoke na faida zake kwa mwanadamu
Mimea mingi ina faida katika mwili wa binadamu, wanyama na hata mingine kutumiwa kurutubisha udongo. Wengi wetu tumezungukwa na mimea ambayo hatufahamu faida zake, kumbe mimea hiyo ni tiba kwa magonjwa mbalimbali hata yale sugu kama presha na mengineyo. Katika makala hii tutaangazia mmea unaoitwa artichoke. Mkulima Mbunifu katika jitihada zake za kutembelea wakulima ilikutana na mkulima Bwana Kambaga kutoka…
Kilimo ikolojia ni suluhisho la changamoto ya chakula duniani
Mama shujaa wa chakula na mnufaika wa jarida la MkM. Anazalisha kwa kufuata mbinu za Kilimo Ikolojia.
Wakulima Watumia Taarifa za MkM Kuboresha Uzalishaji
Jambo la kufurahisha ni pale unapoona mkulima anajifunza na kutekeleza, hii inatia moyo. Mmoja wa wakulima wanufaika wa jarida la Mkulima Mbunifu ametia fora kwa namna ambavyo amepokea mafunzo ya kilimo ikolojiahai. Mbinu mbalimbali zilizoandikwa zimejipatia umaarufu mkubwa miongoni mwa wakulima kiasi cha kuanza kutekeleza mara moja, ni pamoja na utunzaji wa udongo, matumizi ya mbolea na madawa ya asili,…
Vyanzo vya virutubisho
Ni vyema kujenga uelewa wa vyanzo vya virutubisho vinavyoweza kutumika katika kilimo hai. Uelewa wa maisha ya mimea husaidia kwa kiasi kikubwa kwa hatua ya kuchukua kuilisha mimea hiyo. Kuna mwingiliano kati ya uzalishaji wa mimea na mifugo na unachangia katika kurutubisha udongo. Mabaki ya mazao hulisha wanyama na samadi ya wanyama hurutubisha udongo. Pia, mifugo hao, kama madume, wanaweza…