Kilimo

- Kilimo, Udongo

Zifahamu kanuni za kilimo ikolojia kwa uzalishaji wenye tija na lishe bora

Kilimo ikolojia ni njia ya kilimo inayolenga kuhifadhi mazingira, kuhimiza uendelevu, na kukuza ustawi wa jamii kwa kuzingatia mifumo ya ikolojia na utamaduni wa eneo husika. Ni mfumo ambao unazingatia uhusiano wa karibu kati ya mimea, wanyama, binadamu, na mazingira yao, na kujaribu kuiga mifumo ya asili ili kudumisha bioanuai na kuzuia uharibifu wa mazingira. Kanuni na vipengele 13 vya…

Soma Zaidi

- Kilimo

Faida na matumizi ya mbolea ya kijani

Mazao ya mbolea ya kijani ni mazao ambayo yanapandwa ili kuongeza rutuba kwenye udongo. Mazao ya mbolea ya kijani ya jamii ya mikunde (ambazo ni zile zinatengeneza mbolea ya naitrojeni kutoka kwenye naitrojeni iliyopo kwenye hewa) zinaweza kuwapa wakulima wadogo faida nyingi sana ikiwa ni pamoja na: Zinatoa kiasi kikubwa cha naitrojeni kwa ajili ya udongo, Zinaongeza tani nyingi za…

Soma Zaidi

- Kilimo

Biashara inahitaji mpango thabiti

Miaka ya hivi karibuni serikali pamoja na wadau wengine wamekuwa na mikakati thabiti ya kuwashawishi wakulima kuweka shughuli zao katika mtazamo wa kibiashara. Waliochukua na kuufanyia kazi ushauri huo kisha kufanya shughuli za kilimo, kitaalamu kwa mtazamo wa kibiashara leo wanapata faida kubwa. Faida hiyo haiji kirahisi. Kuwa na wazo ni aina gani ya kilimo unayoweza kuifanya kibiashara pekee haitoshi.…

Soma Zaidi

- Kilimo

Tumbaku kwenye mbogamboga

Tumbaku ni dawa ya asili inayoweza kutumika katika kilimo cha mbogamboga Tumia ugoro au chemsha miche 20 ya tumbaku. Dawa hii inazuia wadudu wanaoshambulia mahindi shambani, wadudu wanaokata miche, kupe, vidukari, viwavi na wengine. Chukua gramu 500 za tumbaku, changanya maji lita nane na uchemshe. Chuja baada ya kupoa, ongeza maji lita nane tena na gramu 60 za sabuni ili…

Soma Zaidi

- Kilimo

Kitunguu saumu kama dawa ya asili

Kitunguu saumu pia kinaweza kuwa mbadala wa kudhibiti viwavi, nzi wa matunda, utitiri mwekundu, utitiri mweupe, wadudu wenye magamba laini, kombamwiko wa madoa, magonjwa ya fangasi na minyoo fundo. Menya kilo mbili za kitunguu saumu na uzitwange vizuri (tumia blenda ni vizuri zaidi). Ongeza mililita 500 za maji ili kusaidia kukamua juisi/ mchanganyiko. Tumia chujio kupata mchanganyiko wa kitunguu saumu.…

Soma Zaidi

- Kilimo

Dawa za asili kwa uzalishaji wa mbogamboga

Uzalishaji wa mboga mara nyingi unahusisha matumizi ya viuatilifu vyenye kemikali. Baadhi ya wakulima hawawezi kumudu gharama kubwa za viuatilifu hivi, ambavyo visipotumika vizuri huweza kuleta madhara, kama kuharibu mazingira, mimea na kuathiri watumiaji wa mboga. Njia asilia za kudhibiti visumbufu hutumia dawa zinazotokana na mimea ambayo hupatikana katika maeneo ya wakulima. Matumizi ya dawa hizi ni njia mojawapo ya…

Soma Zaidi

- Kilimo, Udongo

Kudhibiti afya ya udongo ni mojawapo ya njia rahisi na mwafaka zaidi kwa wakulima kuongeza uzalishaji wa mazao na faida huku wakiboresha mazingira.

Udongo wenye afya ndio msingi wa kilimo chenye tija na endelevu. Kusimamia afya ya udongo kunaruhusu wazalishaji kufanya kazi na ardhi – sio dhidi ya – kupunguza mmomonyoko wa ardhi, kuongeza upenyezaji wa maji, kuboresha baiskeli ya virutubishi, kuokoa pesa kwenye pembejeo, na hatimaye kuboresha ustahimilivu wa ardhi yao ya kufanya kazi. Iwe unalima mahindi, unafuga ng’ombe wa nyama, au…

Soma Zaidi

- Kilimo, Udongo

Kilimo hai kwa vitendo

Mtazamo Virutubisho hai Mbolea zisizo za asili hazitumiki katika kilimo hai. Virutubisho vya asili vinavyotokana na mimea hutumika kurutubisha udongo. Kuongeza rutuba kwenye udongo huchukuliwa kama nguzo muhimu. Mbolea za asili hutumika kuboresha au kushikilia rutuba ya udongo, kwa kuongeza mbolea inayotokana na mifugo, mbolea vunde, na kuacha mabaki ya mazao shambani yatumike kama matandazo. Mbolea za asili huwa na…

Soma Zaidi

- Kilimo, Udongo

Fahamu kuhusu kilimo hai na namna ya kuanza

Kwa kawaida viumbe hai vyote ni vya asili. Fikra na mitazamo juu ya kilimo hai inaonekana kama vile viumbe hai wana sehemu yao maalumu tangu miaka mingi iliyopita. Hii inajumuisha viumbe wadogo wadogo waliopo ardhini, kwenye mimea, wanyama pamoja na binadamu mwenyewe. Mfumo wa kilimo hai umetelekezwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko katika sekta ya viwanda, ongezeko la watu na…

Soma Zaidi

- Kilimo

Katika kilimo cha sasa, mkulima ni mzalishaji na muuzaji

Wakulima wanalalamika kwamba hawawezi kupata soko ya mazao yao. Katika dunia ya sasa, teknolojia ya habari na masawasiliano, uboreshaji wa miundo msingi ya usafiri na uchukuzi, ikiwemo barabara, soko imeanza kubadilika kuliko awali. Soko imeanza kuwa wazi na yenye ushindani mkubwa, na hii inatoa fursa kwa wakulima wadogo, hasa wale wa kilimo hai ambao wana uwezo wa kutumia mtandao, yaani…

Soma Zaidi