- Binadamu

Zingatia usalama wa chakula kipindi hiki cha ugonjwa wa COVID-19

Sambaza chapisho hili

Janga la Covid-19 linachangia changamoto ya usalama wa chakula na lishe bora duniani. Kuwepo na mfumo endelevu wa chakula na mahali panapoweza kuhakikisha usambazaji wa chakula bora katika nyakati kama hizi, ni fursa ambazo miji michache ulimwenguni zinafurahia. 

Nchi nyingi na mashirika yanaongeza jitihada za kufanya kilimo salama, ili kupambana na changamoto za usalama wa chakula, ambao unaweza kusababisha janga la njaa kutokana na vizuizi vilivyowekwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19.

Chakula ni hitaji la muhimu katika mwili wa binadamu. Kiwango cha afya, kustawi kimwili na kiakili, utulivu wa kiroho, kupata uwezo na nguvu, kuongeza kizazi na kadhalika. Yote hayo kwa njia moja au nyingine yanategemea afya bora na usalama wa chakula.

Usalama wa chakula ni nini? 

Usalama wa chakula maana yake, watu wote katika jamii wanaweza kupata chakula cha kutosha na katika kipindi chote cha maisha hai. Kaya inachukuliwa kuwa na chakula wakati wakaazi wake hawaishi kwa njaa au hofu ya njaa. Hata hivyo, patikanaji

wa chakula, matumizi ya chakula cha kaya.

Na kwa nini tuzingatie usalama wa chakula kipindi hiki cha COVID-19 

Ni muhimu, pia ni jukumu la kila mwanajamii kuzingatia usalama wa chakula, hasa katika kipindi kama hiki ambacho watu wengi wameingiwa na hofu, ambayo kwa namna moja au nyingine inaathiri mfumo wa uzalishaji wa chakula. Ni vyema kuanza kuhakikisha chakula kinakuwa endelevu na kinapatikana kwa urahisi pale kinapohitajika.

 Uwepo wa chakula unasaidia kutatua yafuatayo;

 Kuzuia athari kama vile kuwepo na baa la njaa

  • Kuimarisha afya za wanajamii kama kuzuia utapiamlo,
  • Huchangia kuongeza nguvu kazi ya ujenzi wa taifa
  • Hupunguza umaskini ambao unaweza kusababisha matumizi yasiyoendelevu ya mali asili.

Nafasi ya mkulima

Mkulima ana nafasi kubwa katika kuhakikisha usalama wa chakula kuanzia ngazi ya familia, kijamii, kitaifa na kimataifa.

Mambo kadhaa yanatakiwa kuzingatiwa; 

Kuotesha mazao sahihi kwa msimu husika na yanayoweza kutumiwa na jamii.

  • Fuatilia njia sahihi na salama za uhifadhi wa mazao ili yasiharibike, ikiwa ni pamoja na kuongeza mnyororo wa thamani ili kupata bidhaa itakayohifadhiwa muda mrefu.
  • Zingatia njia sahihi na salama za usafirishaji wa mazao kwenda sokoni.
  • Fuatilia taarifa za masoko kupitia vyanzo mbalimbali za habari kama redio, television, mitandaoni, vibao vya matangazo katika vituo vya masoko, halmashauri za miji na wilaya mbalimbali na kadhalika.

MUHIMU: Wakati hayo yote yakifanyika, mkulima unasisitizwa kuhakikisha usalama wako na jirani yako juu ya maambukizi ya virusi vya Corona. Mueleimishe jirani yako juu ya ugonjwa wa Corona, maambukizi na namna ambavyo ugonjwa huu umeathiri sekta mbalimbali za kiuchumi ikiwamo sekta ya kilimo.

Fuatilia taarifa za habari kwani serikali kupitia wizara ya afya inatoa taarifa mara kwa mara juu ya ugonjwa huu wa COVID-19, hivyo ni vyema kujua kinachoendelea na kujiweka sambamba na yanayoendelea.

 

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *