- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara

Zalisha kwa malengo ili kupanua kilimo biashara

Sambaza chapisho hili

Kama kawaida jarida hili linatoa wito kwa wakulima kuanzisha na kujenga kilimo kuwa biashara inayoweza kuleta faida na kukidhi mahitaji ya kila siku hapo nyumbani. Hata hivyo, imekuwa ni kawaida kwa wakulima wengi kufanya shughuli zao bila kufanya maandalizi thabiti, na bila kuwa na mipango itakayowawezesha kupanua uzalishaji na kuifanya kuwa endelevu.

Swala hili ni kikwazo kikubwa sana kwa sababu hautaweza kufanya kazi zako kwa malengo unayoyajua, kuelewa na uliyoyaweka tangu mwanzoni. Utakuwa mtu wa kuchukua kila linalokuja mbele yako, na mwishowe unajikuta haujaweza kufanya jambo la maendeleo na kutokufikia malengo pia.

Kama haukufanikiwa kuyafikia malengo yako mwaka huu, usikate tamaa. Kuna msemo usemao tunajifunza kutokana na makosa, hivyo, kuna nafasi katika mwaka unaokuja ya kuibua mipango yako, kuyafanyia kazi na kupata mafanikio mazuri. Na kama umefanikiwa mwaka huu, utatia fora zaidi ikiwa tayarekebisha makosa madogo yaliyokupata na kuyaimarisha yaliyokuletea fanaka.

Ni vyema sasa kujipanga na kufanya maandalizi: kuwa ni kilimo cha namna gani utafanya, ni ufugaji wa namna gani unaotaka kufanya, na ni nini malengo yako katika uzalishaji na uuzaji ili kupata bei inayofaa sokoni?

Mkulima Mbunifu linaendelea kuhakikisha kuwa linakusaidia kupata taarifa muhimu kwa kile ambacho umekusudia kufanya, iwe ni kulima au kufuga, pamoja na kukuhimiza kuingia katika usindikaji wa mazao utakayozalisha. Ikiwa hauna wazo la kile unataka kufanya basi soma yaliyomo kwenye jarida hili na bila shaka utapata wasaha kutokana na mafanikio ya wakulima wengine na uhitaji uliopo kwa watumiaji ya mazao ya kilimo.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *