- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Masoko

Tengeneza unga wa mbegu za parachichi na tumia kwa afya

Sambaza chapisho hili

Unga wa mbegu za parachichi

Parachichi ni moja ya matunda maarufu duniani kote. Tunda hili hutumika kwa shughuli mbalimbali, kama vile kuliwa kama tunda, utengenezaji wa mafuta ya kula, vipodozi, n.k. Pia, matawi ya mparachichi yanaweza kutumika kama malisho kwa mifugo, huku mti wake ukitumika kama kuni au hata magogo ya kujengea.

Hivi karibuni imegundulika kuwa mbegu za parachichi zina manufaa makubwa kwa kuwa unga wake hutumika kwa matibabu na pia kama kipodozi.

Matayarisho

  • Kata vipande vidogo vidogo, kisha kausha kwenye kikaushio cha sola ili kulinda virutubisho visipotee.
  • Mbegu hizi huchukua muda wa siku 1-2 kukauka.
  • Saga kwenye mashine maalumu ili kupata unga.

Matumuzi

Unga wa mbegu za parachichi unaweza kutumiwa kwa kuweka kwenye chai, maziwa, uji, au supu. Tumia kijiko kimoja cha chai au itakavyoelekezwa.

Tahadhari: Usizidishe kipimo kwani kwa kufanya hivyo inaweza kusababisha kuharisha.

Changamoto

Elimu zaidi inahitajika kwa wakulima, ili kuweza kubaini ni mbegu zipi zinazofaa kutengeneza aina hii ya unga, kwani si aina zote zinazofaa, jambo ambalo litawaongezea wakulima wadogo wadogo kipato.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *