- Binadamu, Kilimo

Ni muhimu kuhakikisha usalama na kuzuia upotevu wa chakula

Sambaza chapisho hili

Umakini wa uzalishaji huzuia upotevu wa chakula Upotevu wa chakula hutokea katika mnyororo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji.

Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi.

Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla ya chakula kumfikia mlaji. Kwani chakula kinachofaa kuliwa hupotea aidha katika awamu ya uzalishaji, uhifadhi, usindikaji ama kutumiwa kulisha wanyama ama kutengenezea mboji, nishati ya kibaolojia na mbolea asilia. Wakulima wanaweza kutathmini usambazaji.

Hata hivyo mkulima unaweza kupunguza upotevu wa chakula kwa kuboresha ukuzaji wa bidhaa, uhifadhi, uuzaji na hata kutumia mbinu bora katika mapishi. Vile vile mabaki ya chakula au taka yanaweza kutumiwa kulisha wanyama ama kutengenezea mboji, nishati ya kibaolojia na mbolea asilia.

Wakulima wanaweza kutathmini upotevu wa chakula wakati wa usindikaji, usambazaji, na uhifadhi na kutumia mbinu bora.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *