MkM kwenye mtandao wafugaji kwa miaka kadhaa wamekuwa wakifuga kimazoea, bila kuzingatia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wenye tija.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha kiasi Tanzania ni nchi yenye uwezo wa kuzalisha mazao mengi ya chakula na ya biashara. Hii ni kutokana na hali ya hewa nzuri pamoja na udongo wenye rutuba ya asili unaowezesha mazao hayo kukua na kufanya vizuri katika uzalishaji.
Pamoja na hayo, wakulima wengi wakubwa na wadogo wamekuwa wakijikita katika kuzalisha mazao fulani tu mara kwa mara, lengo kubwa likiwa ni kulenga soko. Si vibaya kufanya hivyo lakini ni vyema tukatambua kuwa hatuna budi kujikita katika uzalishaji wa aina mbalimbali ya mazao ya chakula kwa ajili ya kujenga na kulinda afya za wakulima wenyewe pamoja na walaji.
Mara kwa mara watu wengi hasa watoto wadogo wamekuwa wakipoteza maisha na wengine kudhoofika kiafya na kudumaa kutokana na kukosekana kwa lishe bora. Hii yote hutokana na kula vyakula vya aina moja kila wakati hasa vyakula vya wanga kwa wingi na ambavyo havina virutubisho kamili vinavyohitajika mwilini.
Orodha ya mazao na viini lishe vyake
Mazao Viini lishe muhimu
Mtama: fosforasi, chuma, magnesiamu
Mihogo: wanga, vitamini C, nyuzinyuzi
Mahindi ya asili: antioxidants, vitamini B, zinc, nyuzinyuzi
Kunde: folate, chuma, zinki
Choroko: protini, vitamini B9, nyuzinyuzi
Maharagwe ya asili: chuma, protini, folate, potasiamu
Mehe (Mahindi): mafuta ya asili, chuma, protini
Njugu karanga: protini, vitamini E
Alizeti: mafuta yenye afya, vitamini E, selenium
Maboga: vitamini A, C, zinki, nyuzinyuzi
Viazi vitamu: beta-carotene, vitamini C, nyuzinyuzi
Kisamvu: vitamini A, C, kalsiamu
Mlenda: vitamini K, C, chuma
Mnavu: chuma, vitamini A, kalsiamu
Majani ya maboga: vitamini C, chuma
Karoti: beta-carotene, vitamini A
Ndizi mbichi: potasiamu, wanga, vitamini B6
Tende: sukari ya asili, nyuzinyuzi, potasiamu
Embe la asili: vitamini C, A, nyuzinyuzi