- Binadamu, Kilimo

Maharagwe ni chanzo bora cha virutubisho

Sambaza chapisho hili

Maharage sehemu ya familia ya kunde. Mmea wa mikunde hutoa mbegu kwenye ganda; maharagwe ni mbegu zilizokomaa ndani ya maganda haya. Maharagwe ni chanzo cha virutubishi vingi; zina aina mbalimbali za vitamini, madini na virutubisho vingine huku zikitoa kiwango cha wastani cha nguvu (carbohydrates).

Maharage ni chanzo cha protini ambayo husaidia kujenga mwili, nyuzinyuzi ambayo husaidia umeng’enyaji wa chakula, madini ya chuma, potasiamu na magnesiamu na folate ambayo hutumika katika utengenezaji wa damu (na hii ni muhimu kwa watoto, akina mama wajawazito na wanaonyonyesha). Pia, huwa na mafuta kidogo, na madini ya sodiamu. Hivyo, ni chakula muhimu kwa kaya mzima na ambayo inaweza kuzalisha kwa gharama ya chini na wakulima.

Kwa sababu ya mkusanyiko huu wa juu wa virutubishi na kukuza afya ya binadamu, ulaji wa maharagwe zaidi katika lishe ya kaya nyingi Tanzania kunaweza kuboresha afya kwa ujumla na pia kupunguza hatari ya kupata magonjwa fulani. Ni vyema kutumia maharagwe na mikunde kwa ujumla kama chakula mara kwa mara, angalau kikombe 1.5 ya maharagwe kwa wiki ili kufaidika na manufaa haya ya kiafya.

Maharage ni chanzo kikubwa cha nyuzinyuzi mumunyifu na zisizo na maji. Ulaji wa nyuzi katika chakula huchangia hisia za kushiba na husaidia kudumisha utendaji kazi wa mfumo wa usagaji chakula.

Akina mama wajawazito na wanaonyonyesha

Maharagwe yamejaa madini ya foliki (folate). Madini haya ni muhimu kwa uzalishaji wa chembechembe nyekundu za damu katika mwili wa binadamu na ukuaji wa mfumo wa neva katika hatua za mwanzo za ujauzito. Ulaji wa kutosha wa asidi ya foliki hupunguza hatari ya kasoro za akili na mfumo wa neva kwa watoto wachanga. Hata hivyo, Baadhi ya foliki inaweza kupotea kutoka kwa maharagwe na mikunde mingine wakati wa kuloweka na kupika. Inashauriwa kutumia mbinu ya kuloweka na kupika pole pole.

Kwa watoto

Unene wa kupindukia katika utotoni ni tatizo linaloendelea kuongezeka nchini kutokana na aina ya chakula, kutumia kiasi kikubwa ya mafuta ya kupikia na kutofanya mazoezi au shughuli inayohitaji nguvu. Mikakati kadhaa yamependekezwa ili kuzuia na kutibu unene wakati wa miaka ya utotoni, kwa kawaida kulenga kuzuia ulaji wa vyakula vyenye mafuta na kusisitiza vyakula vinavyotokana na mimea, hasa matunda na mbogamboga, katika lishe ya watoto.

Kuweka maharagwe katika lishe ya watoto kunaweza kusaidia watoto kudumisha uzani wenye afya, na pia kukuza afya kwa ujumla.

Watoto wengi hawatumii kiasi kcha kutosha cha nyuzinyuzi katika chakula chao. Kwa sababu ya umuhimu wa nyuzinyuzi katika kuleta hisia ya kushiba, ulaji duniwa nyuzinyuzi unaweza kuchangia pakubwa kula chakula kingi, hivyo kupata unene wa kupindukia. Kutokana na faida ya maharagwe na mikunde kwa afya ya watoto ni vyema kuhakikisha kwamba watoto wanakula maharagwe ya kutosha nyumbani na hata shuleni, hasa darasa la chekechea.

Rangi

Rangi ya koti ya maharagwe yana misombo ambayo huathiri uwezo wa mwili kumeng’enya na kufyonza virutubishi vilivyomo kwenye maharagwe. Maharagwe ya rangi nyekundu, kahawia au nyeusi yana kiasi kikubwa cha misombo kuliko maharagwe nyeupe. Hata hivyo, misombo haya hupotea hupotea wakati wa maandalizi ya kawaida na mbinu za kupika inayotumika.

Bei nafuu

Moja ya faida muhimu zaidi za maharagwe ni uwezo wa familia na wakulima kuzalisha, na walaji kumudu bei. Ikilinganishwa na vyanzo vya protini vinavyotokana na wanyama, maharagwe hayana bei ghali sana, na kuyafanya yaweze kupatikana kwa watu mbalimbali. Hii ni muhimu hasa kwa familia zilizo na bajeti ndogo au uwezo mdogo wa kiuchumi kuhakikisha kwamba watoto na akina mama wanaweza kupata lishe muhimu bila matatizo ya kifedha.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *