Bustani ya nyumbani, ni eneo dogo lililokaribu na nyumba linaloandaliwa na wanafamilia na kupandwa mazao mbalimbali ya mbogamboga kwaajili ya familia. Hata hivyo, katika maeneo mengi wanawake ndio wamekua wakijishughulisha na bustani ndogo za nyumbani.
Mara nyingi bustani ya nyumbani hujumuisha uzalishaji wa mazao ya muda mfupi hasa mbogamboga kwani ni rahisi kuyahudumia kwa gharama nafuu lakini pia yanazalisha kwa muda mfupi na kumpa mlaji au familia uhakika wa lishe bora muda wote.
Kulingana na mafunzo mbalimbali yanayotolewa na MkM, wakulima wengi wameweza kujifunza na kuanzisha bustani ya nyumbani jambo ambalo wanaeleza kuwa imekuwa msaada mkubwa sana kwa kaya zao.
Katika Makala ijayo, tutajifunza ni kwa namna gani baadhi wa wakulima na wanufaika wa jarida la Mkulima mbunifu, walivyoweza kuanzisha na kudumisha bustani za nyumbani.