Upotevu wa chakula hutokea katika wigo mzima wa uzalishaji, kuanzia shambani hadi usambazaji kwa wauzaji rejareja hadi kwa walaji.
Upotevu huo unaweza kusababishwa na ukungu shambani, wadudu, au udhibiti duni wa hali ya hewa; hasara nyingine hutokana na njia za upishi na upotevu wa chakula kwa makusudi.
Upotevu wa chakula husababisha hasara kabla ya chakula kumfikia mlaji. Kwani chakula kinachofaa kuliwa hupotea aidha katika awamu ya uzalishaji, uhifadhi, usindikaji ama usambazaji.
Hata hivyo mkulima unaweza kupunguza upotevu wa chakula kwa kuboresha ukuzaji wa bidhaa, uhifadhi, uuzaji na hata kutumia mbinu bora katika mapishi. Vile vile mabaki ya chakula au taka yanaweza kutumiwa
kulisha wanyama ama kutengenezea mboji, nishati ya kibayolojia na mbolea asilia.
Wakulima wanaweza kutathmini upotevu wa chakula wakati wa usindikaji, usambazaji, na uhifadhi na kutumia mbinu bora.