Hii ni jibini aina ya cheddar ambayo asili yake ni huko Uingereza lakini kwasasa hutengenezwa katika nchi mbalimbali dunian.
Hatua za utengenezaji
- Pima ubora wa maziwa
- Pasha moto maziwa kufikia nyuzi joto 65C yaache katika joto kwa dakika 30 au nyuzi joto 71.5C kwa sekunde 15
- Poza maziwa kufikia nyuzi joto 22 hadi 25C
- Weka kimea cha mtindi (mesophilic) asilimia 0.25 hadi 0.5 ya maziwa yanayotumika.
- Pasha maziwa moto hadi kufikia nyuzi joto 30 hadi 32C
- Acha maziwa yatulie kwa dakika 15, kisha koroga na acha kwa dakika 15 nyingine yakiwa yamefunikwa.
- Weka rennet, koroga na hakikisha nyuzi joto ni 30 hadi 32C na acha kwa dakika 30 ili yagande.
- Kata curd, koroga na ondoa whey theluthi moja
- Pika curd kufikia nuzi joto 38 hadi 40C, kwa dakika 45 huku ukiendelea kukoroga
- Ondoa whey yote
- Rundika curd (cheddaring/matting) acha kwa dakika 15, geuza na rudia tena baada ya dakika 15
- Saga curd kwa mikono (milling) weka chumvi kwa kunyunyizia (salting)
- Weka kitambaa kwenye kifyatulio kisha jaza curd iliyowekwa chumvi (hooping)
- Gandamiza curd kwa kutumia mashine maalumu kwa dakika 45, kwa hali ya kawaida vijijini gandamiza kwa kutumia kitu Kizito kwa saa 24
- Ondoa curd kwenye kifyatulio na tumbukiza kwenye maji ya chumvi kali (brining) ya asilimia 15, kwa muda was aa 12 hadi 24
- Ondoa jibini kwenye maji ya chumvi, halafu weka kwenye kabati ya wavu kwenye chumba kikavu chenye ubaridi na hewa ya kutosha kwa muda wa miezi mitatu
- Paka parrafin wax au cheese wax ili kutunza ubora na baada ya mwezi mmoja jibini itakuwa tayari kwa matumizi
- Hifadhi kwenye jokofu
- Pima uzito wa jibini kisha fungasha tayari kwa soko
- Andika tarehe ya kutengeneza nay a mwisho wa matumizi
- Muda wa matumizi usizidi miezi 12 baada ya kutengeneza
Matumizi
Jibini ngumu hutumika kama kitafunwa na huliwa pamoja na vyakula vingine kama vile mkate na mbogamboga.
Maoni kupitia Facebook