Nyanya chungu (ngogwe)
- Chagua sehemu ya kufanyia kazi
- Chagua ngogwe zilizokomaa vizuri
- Osha ngogwe kwa maji safi
- Kata vipande kwa wima (Vertically)
- Kata vipande vyembamba vyenye unene wa milimita 2-3
- Tumbukiza vipande vilivyokatwa ndani ya juice ya maji ya limao ili kutunza rangi yake ya asili.
- Panga katika matrei tayari kwa kukausha
- Kausha kwa muda wa siku tatu hadi ifikie kuwa kama ngozi.
Mbogamboga jamii ya majani
Majani ya maboga na mchicha
- Chagua majani mabichi na laini
- Chambua mboga na kuondoa nyuzinyuzi
- Osha majani yako kwa maji safi
- Tumbukiza mboga kwenye maji ya vuguvugu kwa dakika 3-5 ,kisha weka mboga kwenye maji ya baridi Kwa dakika 1 ipoe ili kuzuia kue-ndele kuiva zaidi
- Toa na iache mboga ichuje maji
- Weka katika matrei tayari kwa kukausha
- Kausha mboga ikauke vizuri kwa muda wa siku 3 (pia itategemea hali ya hewa husika)
Viazi vitamu
- Chagua viazi bora (smooth and firm), osha vizuri kwa maji safi
- Vukiza viazi kwenye maji ya moto hadi viwe laini (30-40) dk
- Vimenye viazi vyako
- Katakata vipande vyenye ukubwa wa (3-5) mm.
- Panga katika matrei tayari kwa kukausha.
- Kausha mpaka kufikia hatua yakuvunjika.
Maoni kupitia Facebook