- Mifugo

Ulaji wa bamia na faida zake mwilini

Sambaza chapisho hili

Moja ya zao lenye faida mwilini ni bamia kama tunda mboga kwani linaweza kukutoa katika hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa sababu ya uwezo wake wa kusaidia kuyeyusha au kumeng’enya sukari na kuuweka sawa mfumo wa sukari mwilini.

Mara nyingi tumekuwa tukichukulia bamia kama mboga ya kimasikini pasipo kujua kuwa bamia ni tunda mboga lenye faida nyingi sana mwilini au kiafya.

Faida za bamia kiafya

  • Moja wapo ya faida ambayo ni muhimu ni kusaidia kumeng’enya sukari mwili au kuweka sawa mfumo wa sukari mwilini.
  • Bamia ni aina ya tunda mboga lenye utajiri wa makapimlo ambayo ni muhimu sana katika mwili hasa katika usagaji wa chakula.
  • Aidha, kukosa choo ni tatizo la kawaida kwa wagonjwa wa kisukari hasa kwa ambao bado hawajua jinsi ya kudhibiti kiwango chao cha sukari katika damu. Bamia ikiliwa mara kwa mara inasaidia kurekebisha mfumo wa umeng’enya chakula na sukari mwilini kisha kuondoa tatizo hili.
  • Maji maji yanayotoka katika Bamia yana uwezo wa kuondoa lehemu katika mishipa ya damu kwenye mwili. Lehemu ni aina ya mafuta yanayopatikana kwenye mishipa damu,endapo mafuta haya yakazidi huweza husababisha maradhi ya shinikizo la damu hivyo mgonjwa wa kisukari mwenye shida ya lehemu ni muhimu sana kula bamia mara kwa mara.
  • Mgonjwa wa Kisukari anahitaji kula aina ya vyakula vyenye virutubisho vya kutosha na bamia imejaliwa kuwa na virutubisho vyenye protini tofauti na matunda mboga mengine au lishe nyingine zenye asili ya mimea,.
  • Mbali na hayo, bamia ina utajiri mkubwa wa virutubisho na vitamin A na B ambavyo kazi ya vitamin hizi ni kuboresha na kuimarisha uwezo wa macho kuona na kwakuwa moja ya changamoto ya wagonjwa wa kisukari ni uono hafifu, bamia ni tiba kinga nzuri kwa afya ya macho.
  • Bamia humsaidia mama mjamzito pamoja na mtoto aliye tumboni kuwa na afya bora na nzuri. Ulaji wa Bamia kwa mama mjamzito humtoa katika hatari ya kujifungua mtoto mwenye tatizo la kupasuka kwa uti wa mgongo au kuwa na tatizo la mgongo wazi. Washauri Lishe wanasisitiza kuwa mama mjauzito apendelee kula aina ya vyakula vyenye wingi wa makapimlo kama bamia ambavyo pia kusaidia kudhibiti kiwango chake cha sukari na kumuepusha kupata Kisukari aina ya tatu.
  • Bamia huongeza na kuboresha kinga ya mwili hasa kwa watu ambao kinga yao ya mwili imeshuka kama watu wenye maradhi yasiyo ya kuambukiza na hata maradhi ya kuambukiza kama HIV.
  • Bamia sio tu kwa watu wenye hayo matatizo tajwa, pia husaidia watoto katika kuboresha kinga na ukuaji wao. Kwa mujibu wa wataalum lishe, wanasema kuwa watu wengi wamekuwa wanakula bamia kwa kuidharau ila bamia husaidia sana kuzuia magonjwa ya moyo, kwa kuisaidia mishipa ya damu kufanya kazi vizuri.
  • Bamia pia husaidia watu wenye matatizo ya vidonda vya tumbona kudhibiti kabisa tatizo hilo.
  • Matumizi ya bamia kwa wingi husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya tumbo na kuongeza kiwango cha damu mwilini. Watu wengi wanatumia bamia kama dawa ya kuongeza kinga ya mwili kwa kutafuna zikiwa mbichi au kuzichemsha.

Angalizo

Kwa wagonjwa ambao tayari wanaumwa kisukari, wasiache dawa zao na kuanza kutumia bamia kama dawa, bali watumie bamia mara kwa mara kama tunda mboga ambalo inasaidia kumeng’esha sukari mwilini na kuimarisha kinga ya mwili wako huku wakiendelea na dawa zao.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

9 maoni juu ya “Ulaji wa bamia na faida zake mwilini

    1. Habari Alwina
      Hongera sana kwa kufuatilia makala mbalimbali za jarida la Mkulima Mbunifu.

      Kuhusu bamia kama dawa ya vidonda vya tumbo, unahitajika kuila mara kwa mara kama chakula yaani mboga au kama tunda iwapo utaweza kula, hivyo kila siku uwe na tabia ya kula tunda hili kwa namna utakavyopendelea.

      Karibu mkulima Mbunifu

    1. Habari
      Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa swali lako.
      Ukisema kupata ujauzito unamaanisha nini? Kama inasaidia kupata ujauzito ama inazuia kupata ujauzito?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *