- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara

Umejiandaa kuhudhuria maonyesho ya wakulima maarufu kama Nanenane?

Sambaza chapisho hili
Hakika siku hazigandi, saa nayo inatembeza mshale wake kwa haraka zaidi, hatimaye sasa tumebakiza siku chache sana kuanza kwa maonyesho ya wakulima Nanenane.
Kama kawaida, Serikali kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali, wajasiriamali, watu binafsi na wananchi kwa ujumla wanakuandalia maonyesho ya siku nane ya kilimo, mifugo, uvuvi pamoja na shughuli mbalimbali za kibishara katika kanda mbalimbali nchini.
MKULIMA MBUNIFU kama kawaida nasi hatuko mbali na wewe, tunakuandalia mambo mbalimbali mazuri ambayo unaweza ukajifunza kupitia wadau wetu katika banda letu lengo likiwa ni kukusaidia kupiga hatua katika shughuli zako za kiuchumi.
SHIME: EWE MKULIMA, MFUGAJI, MJASIRIAMALI, MFANYABIASHARA UANZE KUJIPANGA SASA, MUDA NDIYO HUU, HAKIKISHA MWAKA HUU HAUTAKUPITA, NJOO UJIFUNZE, NJOO UONGEZE MAARIFA, NJOO UKUTANE NA WA WADAU MBALIMBALI, NJOO UTANUE WIGO WA BISHARA! KARIBUNI SANAAAA
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *