- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Kutuhusu, Masoko

MAONYESHO YA WAKULIMA NANENANE, EWE MKULIMA, MFUGAJI NA MJASIRIAMALI VIPI UMEJIANDAAJE?

Sambaza chapisho hili

“Hayawi hayawi sasa yamekuwa”. Kama ilivyo ada mwezi wa nane, huwa ni mwezi wenye shughuli nyingi zinazohusiana na kilimo, ufugaji, uvuvi wasindikaji na hata kilimo biashara tangu mwanzoni kabisa mwa mwezi hadi katikati ya mwezi.  Wakulima, wafugaji na wadau wengine hupata fursa ya kukutana katika maeneo mbalilmbali ili kuonesha kazi zao pamoja na kushirikishana uzoefu katika suala zima la kilimo na ufugaji.

Wakulima katika kipindi hiki hukutana kwenye maonesho ya Nane Nane ili kuweza kubadilishana uzoefu na kushirikishana fursa mbalimbali zinazoweza kuwapatia ufanisi zaidi katika shughuli zao za kila siku.

Kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma, kwa mwaka 2025 Tanzania itaadhimisha Maonesho ya 32 ya Nanenane yenye hadhi ya kitaifa na kimataifa kwa lengo la kukuza uchumi, kuongeza matumizi ya teknolojia bora na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.

Maonyesho haya yatafanyika katika kanda kuu nane ambazo ni Kanda ya Kati (Nzuguni-Dodoma), Kanda ya nyanda za Juu Kusini (Mbeya-John Mwakangale), Kanda ya Mashariki (Morogoro-Mwalimu Julius Kambarage Nyerere), Kanda ya Kusini (Lindi-Ngogo), Kanda ya Ziwa Magharibi (Mwanza-Nyamhongolo), Kanda ya Ziwa Mashariki (Simiyu-Nyakabindi), Kanda ya Kaskazini (Arusha-Themi) na Kanda ya Magharibi (Tabora-Fatuma Mwasa).

Maonyesho haya yatakayofanyika kitaifa Mkoani Dodoma tarehe 1 hadi 8 Agosti 2025 yamebeba kauli mbiu inayosema “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo Mifugo na Uvuvi 2025” ikiwa nchi inaelekea kwenye Uchaguzi Mku wa Raisi pamoja na viongozi mbalimbali wa nchi.

Mkulima Mbunifu tunatoa pongezi kwa serikali kupitia Wizara ya kilimo na chakula kwa namna inavyofanya bidii kuyaendeleza maonesho haya na kufanya kanda zote kushiriki kila mwaka. Hii ndiyo njia pekee na fursa kubwa kwa wakulima kuweza kujitangaza na kupaza sauti kwa pamoja.

Tunategemea kushuhudia mbinu mbalimbali za uzalishaji, teknolijia rahisi kwa mkulima katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo, usindikaji, ujasiriamali na masoko nk.

Ni rai yetu kuwa wakulima na wafugaji watashiriki kikamilifu na kujipa muda kujifunza na kujionea yale wenzao wameandaa ili kuwa na kesho imara na endelevu katika uzalishaji bora na wenye tija..

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *