- Kilimo, Kilimo Biashara

Unaweza kukausha karoti na kusaga kwa matumizi ya baadaye

Sambaza chapisho hili

Imezoeleka kuwa karoti ni moja ya kiungo maarufu cha chakula, ambacho mara nyingi kinatumika kikiwa kibichi, na mara nyingi hakihifadhiwi kwa muda mrefu.

Tofauti na dhana hii, karoti inaweza kusagwa na kuwa unga, ambao unaweza pia kutumika kama chakula.

Utayarishaji

  • Osha karoti kwa kutumia maji ya moto hadi zitakate.
  • Katakata vipande vidogo vidogo.
  • Kausha kwenye kikaushio cha sola ili kulinda virutubisho visipotee.
  • Kausha kwa muda wa siku 5-7
  • Saga ili kupata unga wa karoti.
  • Fungasha kwenye vifungashio maalumu kwa ajili ya mauzo au matumizi binafsi.

Matumizi

Unga wa karoti unaweza kutumika kwa kuweka kwenye vinywaji kama vile juisi. Pia unaweza kutumika kama kiungo kwa mboga za aina zote, au hata kula unga. Unaweza kutumia vijiko viwili vya chakula kwa mlo wa watu wanne.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *