- Binadamu, Kilimo, Kilimo Biashara, Usindikaji

Namna ya kutengeneza unga wa maboga

Sambaza chapisho hili

Katika jamii yetu, watu huchukulia kuwa boga ni chakula cha watu masikini ambao hawana namna ya kupata chakula kizuri. Hata badhi ya wakulima hawakubali kujiingiza katika kilimo cha zao hili. Ukweli ni kwamba, hili ni zao ambalo lina manufaa makubwa sana hasa kwa afya ya binadamu. Hii ni kwa sabababu tunda la boga lina kiasi kikubwa cha kalishamu.

Boga ni miongoni mwa jamii ya mimea inayotambaa, ambalo hustawi zaidi katika sehemu zenye joto na hata sehemu za miinuko, ingawa zao hili hufanya vizuri zaidi katika ukanda wa chini wenye joto. Zao hili huchukua kati ya miezi 3-4 tangu kupandwa hadi kuvuna.

Namna ya kusindika

  • Baada ya kuvuna maboga kutoka shambani mwako, ni muhimu kufuata hatua zifuatazo ili kuweza kupata unga wa boga.
  • Osha boga vizuri kisha ukate vipande vipande. Inashauriwa kuwa vipande vidogo vidogo ili kurahisisha ukaukaji.
  • Weka kwenye kikaushio kinachotumia mionzi ya jua (sola drier)
  • Kausha kwa muda wa siku 7-14. Hii inategemea na hali ya hewa, wakati wa kiangazi, boga huchukua siku 7 tu kukauka.
  • Baada ya kuhakikisha kuwa boga limekauka kwa kiwango cha kutosha, saga kwa kutumia mashine maalumu ili kupata unga.
  • Baada ya kusaga, chekecha unga huo ili kuondoa vipande vigumu vilivyosalia au taka nyingine zinazoweza kuwa ziliingia wakati wa kuandaa.
  • Fungasha unga kwa vipimo na kwa kutumia vifungashio maalumu tayari kwa kuuza au kwa matumizi.

Ili kupata kilo moja ya unga wa boga, unahitaji kuwa na matunda 7 ya boga. Ambapo kilo 1 ya unga wa boga inauzwa kati ya shilingi za Kitanzania 15,0002,0000. Vijiko 4 vya unga wa boga vinatengeneza uji nusu lita.

Manufaa kwa afya

  • Unga wa boga una manufaa makubwa kwa afya kwani una kiasi kikubwa cha kalishamu.
  • Unga huu unawasaidia kwa kiasi kikubwa watu wenye matatizo ya kusagika mifupa (baridi yabisi).
  • Matumizi ya unga wa boga, unasaidia kurejesha kumbukumbu hasa kwa watu walioathirika na magonjwa ya aina mbalimbali.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *