- Binadamu, Kilimo Biashara

Elimu ya uandaaji sahihi wa vyakula vya asili ni muhimu

Sambaza chapisho hili
  • Epuka kutengeneza loshoro itakayokaa muda mrefu sana kwenye kibuyu na kuendelea ongeza maziwa.
  • Epuka kuloweka mahindi kwa muda mrefu na kutwanga kwa matumizi hii hupoteza nguvu na ubora wa wanga.
  • Kuosha mahindi au maharage kwa kutumia magadi, hakikisha utayapika kwa kuongeza viungo au kutumia mboga za majani pembeni ili kurudisha virutubisho ulivyopoteza.

Kuna baadhi ya vyakula hutumiwa sana nchini Tanzania kama vile ugali dona, makande, chapati, mboga za majani lakini havitumiki kwa usahihi kwani vinatakiwa kuongezwa thamani.

Vyakula hivi vinaweza ongezewa thamani zaidi kwa kuongeza ubora

  1. Ugali; tuache dhana ya kutumia ugali wa mahindi peke yake unaweza changanya mahindi na mbaazi/ njugu mawe/ boga. Hapa tunapata ongezeko la protini kwenye ugali wetu hata vitamini zingine kama B
  2. Makande; tumezoea kuchanganya mahindi na maharage tu ila unaweza weka mahindi, maharage, mbaazi, njugu mawe, ngano na karanga pia na viungo kama karoti, kitungu na nyanya. Hapa tunakuwa na mlo kamili
  3. Chapati; tumekuwa na tabia ya kupika kutumia ngano peke yake bali unaweza changanya na boga au kiazi lishe hii inasaidia kupata vitamini A zaidi
  4. Mboga za majani; kwa mazoea zaidi huwa viungo kama karoti na kitungu huwekwa kwa kiasi kidogo ila tunaweza ongeza kiwango cha hivi viungo ilikuwa na mboga zenye kiwango kikubwa cha virutubisho lakini ni vyema katika mapishi ya mboga kuchanganya mboga za aina mbalimbali, unaweza pia kuongeza nyama ya ng’ombe, kuku au mbuzi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Afisa lishe kutoka shirika la Iles De Paix (IDP) Monica Michael Morrison.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *