Vanila ni zao la biashara ambalo asili yake ni mexico zao hili limekua likilimwa na kuzalishwa huko mexico, marekani na bara Hindi kwa karne nyingine.
Hivi sasa, zao hili linalimwa maeneo mengi barani Afrika ikiwamo nchi ya Tanzania, japo kwa uchache kutokana na ugumu wake wa kulizalisha, ingawa bei yake ni kubwa sana na wakulima waliofanikiwa kuzalisha wamekuwa wakipata kipato kizuri.
Miche ya vanila nchini
Wakulima wamekua wakihangaika kutafuta miche ya vanilla kwa juhudi kubwa sana, ambapo hapa nchini Tanzania inapatikana kutoka mkoa wa Kagera, na pia huagizwa kutoka nchi jirani ya Uganda.
Aidha, Mkulima Mbunifu imefanikiwa kukutana na mkulima wa vanilla mkoani Arusha, Bi. Penina Mungure ambaye ni mfugaji mkulima na anayetumia mbinu za asili katika kufanya kilimo.
Bi. Penina mbali na kulima vanilla, pia analima zao linguine la kibiashara ambalo ni strawberry pamoja na kufuga kuku, nguruwe, kanga na ngombe.
Mama huyu kwa jina maarufu ‘mama kipande’ anayeishi kijiji cha Kilala, wilaya ya Arumeru, anaeleza namna bora ya kuandaa miche ya vanila pamoja na uoteshaji wake, akiwa ni miongoni mwa wakulima wachache mkoani Arusha wanaootesha miche ya vanila na kuiuza.
Uandaaji wa miche ya vanila
Kama ilivyo kwa mimea aina nyingi ambazo ni lazima kupitia katika hatua ya awali ya miche, vanila nayo ni miongoni mwa zao ambalo ni lazima kuandaliwa miche kwa hatua sahihi.
Mahitaji
Katika undaaji wa miche ya vanila mkulima anatakiwa kuwa na mbolea ya mboji, viriba vya kuoteshea pamoja na mbegu ya vanilla yaani vipandikizi.
Uchaguzi wa vipandikizi
Wakati wa kuchagua vipandikizi vya vanila inayofaa kuotesha, angalia tawi ambalo lilisha zaa au lililokomaa vizuri. Matawi hayo ndio yana uwezo wa kutoa chipukizi na pia hayana kazi kwani hayana uwezo wa kuzaa tena, na utahitajika kuhesabu pingili 5 kisha ukate.
Angalizo: Ukikata tawi ambalo halijazaa au kukomaa, litaathiri uzalishaji wa vanilla katika mmea huo.
Uoteshaji
Chukua viriba jaza udongo (mboji) kutegemeana na namba ya miche unayotaka kuotesha.
Chukua vipandikizi (marandu) yenye pingili tano (5), fukia pingili mbili kwa mfumo wa C ya kutizama juu, acha pingili moja ya mwisho ikae juu bila kufukiwa na pingili mbili za juu kwaajili ya kutoa vichipukizi. Yaani hesabu pingili ya kwanza kutoka chini isifukiwe, ya pili naya tatu ifukie, alafu pingili ya nne naya tano zitizame juu.
Umuhimu wa kuacha pingili moja bila kufukia
Pingili moja unayoiacha bila kufukiwa inasaidia kukuonyesha hali halisi ya maendeleo ya mche wako wakati zile pingili mbili zinategemewa kutoa kichipukizi.
Mche ukianza kutoa vichipukizi chukua vijiti vyembamba vya mwanzi chomekeza kwenye kiriba, ili uweze kufunga kichipukizi, kijishikize kiweze kupanda juu.
Mche utachukua miezi mitatu (3) hadi sita (6) inakua tayari kwa mbegu maana mche utakua tayari na urefu wa mita moja na nusu (1 ½M) had mita mbili (2M) na huu ndio unaohitajika kwa mbegu tayari kupelekwa shambani.
I appreciate this page. Am learning a lot from it
Hi Rehema
Thanks for appreciation and you are most welcome to Mkulima Mbunifu. Are you doing farming activities?
Nahitaji mbegu ya vanila
Habari, Karibu Mkulima Mbunifu.
Wewe unapatikana wapi? Na je, umepata elimu sahihi ya kilimo cha vanilla? Kuanzia uoteshaji, uvunaji, uhifadhi pamoja na gharama zake ikiwa ni upatikanaji wa mbegu bora, utunzaji wa shamba la vanilla? Nauliza hivi isijekuwa unataka tu kuingia kwenye kilimo cha Vanilla na hufahamu lolote kuhusu vanilla, unaweza kujikuta unaingia kwenye hasara.
Karibu