- Binadamu, Mifugo

Namna ya kutayarisha maziwa mtindi

Sambaza chapisho hili

Maziwa ya mtindi ni maziwa mabichi ya ng’ombe yaliyoganda na mara nyingi yanakuwa na hali ya uchachu. Maziwa haya hutumika kama kinywaji au kiambaupishi katika mapishi mbalimbali.

Mahitaji

  • Maziwa mabichi safi na salama
  • Kimea cha maziwa

Vifaa vinavyohitajika

  • Sufuria / keni safi ya kuchemshia
  • Chombo (container) ambacho utaweza kuhifadhi mtindi unaoendelea kuchachuka (fermenting) na kiwekwe katika hali ya usafi ili kuwezesha vijidudu hatari visiweze kuwepo na mtindi uendelee kufanya kazi vizuri. Chombo hiki kifunikwe kwa mfuniko safi.
  • Safisha vyombo hivi viuri na usuuze kwa maji ya moto kabla ya kuanza
  • Na kama utaweza kupata kipima joto cha kupikia (Cooking thermometer) basi unaweza kukitumia pia.

Namna ya kutayarisha mtindi

  1. Chemsha maziwa kwa kutumbukiza sufuria yenye maziwa ndani ya sufuria lenye maji yanayochemka mpaka yafikie nyuzi joto la sentigredi 850C na kuyaacha yakiendelea kuchemka kwa dakika 30. Hakikisha unakuwa makini kuangalia maziwa yako na kuyakoroga wakati wote yanapokuwa yanachemka. Na kama utakuwa na kipima joto basi utaweza kutambua kama maziwa yako yamefikia nyuzi joto 850C.
  2. Yaondoshe kutoka kwenye jiko na yaache yapoe mpaka kufikia nyuzi joto 25-300C. Hivyo kuwa na bafu la maji ya baridi litasadidia kupooza joto hili sawasawa na haraka na kuhitaji tu kukorogwa kwa muda Fulani. Kwa nyuzi joto 25-300C unaweza kutambua kwa kuhisi joto la chombo husika kuwa chini kidogo na joto la kawaida la
  3. Weka kimea (Starter Culture) kwa kiwango sahihi (kama ulivyoshauriwa na mtaalam) kwenye lita zako za maziwa zilizopo katika chombo safi ulichokitayarisha kwa ajili ya kuvundika (incubation) na ukoroge vizuri kwa dakika 3-5
  4. Funika chombo na ukiweke sehemu ya joto la wastani (kuvundika) kwa masaa 16-18 ili kuwezesha bakteria waliomo katika mchanganyiko huu waweze kukua (joto linalopasa kutumika likaribie nyuzi joto 25- 300C ikiwezekana).
  5. Baada ya masaa 16 pima mtindi wako kama uko tayari kwa kuangalia uchachu unaouhitaji katika mtindi wako na nyamanyama zilizojitengeneza na kujiridhisha kua mtindi wako uko tayari.
  6. Pooza mtindi wako katika jokofu ili yagande vizuri na kama hutaweza kuhifadhi kwenye joto la kiwango cha chini (jokofu) basi itakulazimu kutumia kwa siku moja tu.

Dozi ya culture

  • 1Packet ni kwa lita 500-600 za
  • 1kijiko cha chai (wastani) ni kwa lita 100
  • ½ kijiko cha chai ni kwa lita 50
  • ¼ kijiko cha chai kwa lita 20- 25
  • 1/8 kijiko cha chai kwa lita chini ya 20
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *