- Kilimo

Dawa za asili

Sambaza chapisho hili

Majivu

  • Weka majivu moja kwa moja kwenye mashina ya mimea michanga baada ya kuotesha ili kuzuia wadudu wakatao mimea kama vile sota (cutworms).
  • Majivu yataonyesha matokeo mazuri endapo yatachanganywa na mafuta ya taa kidogo

Pilipili kali

  • Chukua gramu 55 za pilipili kisha katakata
  • Chemsha kwa dakika ishirini kwenye maji lita 5.
  • Chuja kisha ongeza maji lita 5.
  • Dawa hii huua wadudu wenye ngozi ngumu (mbawa kavu) na laini, mfano, vidukari, wadudu wa kabeji na kadhalika.

Vitunguu saumu

  • Hutumika kwa kufukuzia wadudu kutokana na harufu yake.
  • Chukua gramu 100 za vitunguu kisha vitwange.
  • Changanya na maji lita 2.
  • Chuja kisha nyunyizia kwenye mimea.
  • Pia, dawa hii inaweza kuchanganywa na mojawapo ya dawa za asili ili kutoa harufu kali itakayofukuza wadudu.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *