Wanajamii wengi hawatambui umuhimu wa miti katika kilimo, mazingira, kwa binadamu na hata kwa wanyama jambo ambalo wengi wamelipuuzia na kutokulichukulia maanani. Tunapozungumzia miti, kwa ujumla tunamaanisha miti ya asili ambayo zipo katika misitu yetu na hata maeneo yetu ya makazi pamoja na ile ya kuotesha inayotupatia rutuba ya udongo, hewa safi, chakula cha wanyama, kivuli, mbao, kuni, madawa…
