- Kilimo, Mifugo

Vidokezo muhimu kwa wakulima na wafugaji

Sambaza chapisho hili

Ng’ombe wangu anapata choo kigumu sana na mara nyingine, kinaambatana na ute kama makamasi na damu, huu ni ugonjwa gani, na nasikia kuna dawa za kienyeji zinazotibu! Ni dawa gani, na
inaandaliwaje? Msomaji MkM

Kuna uwezekano mkubwa kuwa ng’ombe wako anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama ndigana baridi au kitaalamu Anaplasmosis.

Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakte- ria ambapo mnyama hujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na makamasi kama ulivyo eleza katika swali lako.

Pia huwa na homa kali kiasi cha kufikia nyuzi joto 42. Kukosa hamu ya kula, na hatimae hufa baada ya siku nane kama hatatibiwa mapema. Njia za asili ambazo unaweza kutumia kumtibu mnyama mwenye dalili au kugundulika kuwa na ugonjwa wa ndigana baridi ni pamoja na kutumia mmea unaojulikana kama mpungate/kakati au kitaalamu Opuntia exaltata.

Dawa hiyo husaidia kulainisha tumbo la mnyama na kuuwa bakteria wote wanaosababisha ugonjwa huo kwa mnyama husika.

Namna ya kutayarisha

  • Chukua majani kadhaa ya mpungate/kakati.
  • Safisha.
  • Katakata vipande vidogovidogo.
  • Twanga kwenye kinu hadi yalainike.
  • Weka maji kiasi.
  • Chuja ili kubakia na juisi peke yake.
  • Changanya na maji kiasi.

Matumizi
Mnyweshe ng’ombe mgonjwa kiasi cha milimita mia saba (700ml), yaani kwa lugha rahisi chupa mbili za bia. Rudia hatua hiyo kwa muda wa siku tatu mfululizo, mnyama atapona kabisa.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *