Wafugaji walio wengi, hudhania kuwa wanyama hawana hadhi ya kufanyiwa usafi au kuwekwa katika mazingira safi kama ilivyo kwa binadamu. Hata kama viwango hutofautiana, lakini ifahamike kuwa mifugo pia inastahili kuishi katika mazingira ambayo ni safi na salama.
Kwa kufanya hivyo, itasaidia kuepusha wanyama kushambuliwa na magonjwa ya aina mbalimbali ikiwepo magonjwa ya ngozi yanayosababishwa na vimelea vinavyotokana na uchafu.
Moja ya magonjwa ambayo ni hatari sana kwa wanyama yanayotokana na uchafu, ni pamoja na magonjwa ya ngozi na yale yanayosababishwa na minyoo.
Ni jambo la busara sana kuhakikisha kuwa mifugo ipo katika mazingira safi na salama wakati wote.