Kumekuwa na mfumko wa watu wengi mijini na vijijini kuingia katika ufugaji wa samaki. Miradi hii huwagharimu fedha nyingi, lakini hufa baada ya muda mfupi.
Ili mfugaji aweze kuwa na ufugaji wenye tija, hana budi kujifunza ufugaji wa samaki kwa njia ya kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vifaa vingine vinavofanana na hivyo, vyenye uwezo wa kufugia samaki.
Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo. Aina hizo za samaki hujumuisha aina ambazo sio samaki wanaozaliana na wale wanaozaliana.
Ni dhahiri kuwa mfugaji ata-pata urahisi endapo atafuga samaki wasiozaliana. Hii ni kwa sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana atalazimika kuwa na utaratibu wa kuhamisha vifaranga kwenda sehemu nyingine, mfano bwawa lingine.
Nini mahitaji katika aina hii ya ufugaji?
Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la a-rdhi, maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.
Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa liwe. Bwawa linaweza kuwa la kujenga kwa kutumia saruji (cement), kutandika nailoni (plastic) au la kuchimba tu. Bwawa huchimbwa au kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi.
Aina ya samaki wanaofugwa zaidi
Kuna aina nyingi zaidi za samaki wafugwao katika maeneo mbalimbali hapa nchini, na duniani kwa ujumla. Miongoni mwa samaki hao ni pamoja na Sato, Kambale na aina nyinginezo ambazo hufugwa kwa wingi zaidi.
Kiwango cha samaki kwa eneo
Ili kuwa na ufanisi, unahitaji samaki 7-8 katika mita moja ya mraba. Hii ina maanisha kwamba kama una mita za mraba 600, basi unaweza kufuga samaki 4,500.
TAHADHARI: Haishauriwi kuru-ndika samaki kwenye eneo ndogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa safi ya oxygen.
Ni nini kifanyike ili kuwa na hewa ya kutosha kwenye bwawa?
Zipo njia nyingi za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye ma-bwawa. Ukishachimba bwawa, (aidha na kulijengea), ingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa.
Ni lazima kumwagia chokaa kwenye bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua vimelea kama bakteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako. Unahitajika kurutubisha maji hayo kwa kuchanganya na mbolea.
Unaweza kutumia mbolea kama ya ng’ombe na mbolea za viwandani, ingawa haishauriwi sana kutumia mbolea za viwandani).
Baada ya kutumia mbolea ina-shauriwa kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi. Hii ni kwa ajili ya kuweka mazingira ya ute-ngenezaji wa chakula cha asili kwa ajili ya samaki kujitengeneza. Vyakula hivyo huwa katika hali ya mimea na viumbe wadogo.
Vifaranga vya samaki
Upatikanaji wa vifaranga vya samaki mara nyingi huwa ni mgumu. Hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato. Cha-ngamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo ina hali nzuri.
Vifaranga wataweza kuwa samaki wenye uzito wa kutosha katika kipi-ndi cha miezi sita (6). Hii inamaa kuwa katika kipindi hicho awe angalau na uzito wa gramu 500 au zaidi.
Ukuaji wa haraka wa samaki wako na kuwa na uzito unaotakiwa, hutokana na ulishaji wa vifaranga.
Chakula kinategemena na uzito wao, kwa mfano samaki hula 5% ya mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.
Hapa tunazungumzia ulishaji wa chakula cha ziada, sababu chakula cha asili amekipata kwenye ile mbolea iliyowekwa kwenye bwawa.
Mfano, kama una vifaranga 100 vyenye gramu 10 kila kimoja basi utahitaji gramu 50 kuwalisha.
Katika hali hiyo ya utunzaji mzuri, itakuchukua miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au njia utakayoona inakufaa.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Musa Saidi wa Fish Farming Service Tanzania kwa simu namba 0718986328