Ng’ombe wangu anapata choo kigumu sana na mara nyingine, kinaambatana na ute kama makamasi na damu, huu ni ugonjwa gani, na nasikia kuna dawa za kienyeji zinazotibu! Ni dawa gani, na inaandaliwaje?
Kuna uwezekano mkubwa kuwa ng’ombe wako anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kama ndigana baridi au kitaalamu Anaplasmosis. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria ambapo mnyama hujisaidia kinyesi kilichochanganyikana na makamasi kama ulivyo eleza katika swali lako. Pia huwa na homa kali kiasi cha kufikia nyuzi joto 42. Kukosa hamu ya kula, na hatimae hufa baada ya siku nane kama hatatibiwa mapema.
Njia za asili ambazo unaweza kutumia kumtibu mnyama mwenye dalili au kugundulika kuwa na ugonjwa wa ndigana baridi ni pamoja na kutumia mmea unaojulikana kama mpungate/kakati au kitaalamu Opuntia exaltata.
Dawa hiyo husaidia kulainisha tumbo la mnyama na kuuwa bakteria wote wanaosababisha ugonjwa huo kwa mnyama husika.
Namna ya kutayarisha
- Chukua majani kadhaa ya mpungate/kakati.
- Katakata vipande vidogo vidogo.
- Twangakwenye kinuhadiyalainike.
- Weka maji kiasi.
- Chuja ili kubakia na juisi peke yake.
- Changanya na maji kiasi.
Matumizi
Mnyweshe ng’ombe mgonjwa kiasi cha milimita mia saba (700ml), yaani kwa lugha rahisi chupa mbili za bia. Rudia hatua hiyo kwa muda wa siku tatu.
Asante kwa Elimu
Karibu sana Mkulima Mbunifu