- Mifugo

Ongeza lishe kwa kutumia njia rahisi za ufugaji samaki

Sambaza chapisho hili

Ufugaji wa samaki ni moja ya shughuli ambazo hivi karibuni imejipatia umaarufu mkubwa sana miongoni mwa wafugaji. Kazi hii imekuwa ikifanywa na makundi mbalimbali bila kujali wanafanya shughuli gani nyingine.

Kutokana na uhitaji mkubwa wa lishe inayotokana na samaki, kumekuwa na aina mbalimbali za ugunduzi unaosaidia ufugaji wa samaki kwa njia rahisi.

Katika makala hii tutaeleza ugunduzi mpya wa kutengeneza bwawa rahisi la samaki linaloweza kutumika mahali popote, na familia kujipatia lishe kwa njia rahisi.

Ugunduzi huu uliofanywa na Bw. Semboja Alvin, umewezesha familia mbalimbalikatika wilaya ya Mbulu kurahisisha upatikanaji wa kitoweo.

Aina hii ya ufugaji inamlazimu mfugaji kutumia aina rahisi ya ufugaji ambao huwajumuisha samaki wasiozaliana.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi ambao sio wa kuzaliana(monosexual). Urahisi hapa uko zaidi kwenye kufuga samaki wasiozaliana, kwa sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana inalazimu kuwa na utaratibu wa kuhamisha vifaranga kwenda sehemu nyingine.

Ufugaji wa bwawa rahisi

Hii ni aina ya bwawa ambalo halihitaji kuchimba ardhini au kujengea kwa saruji. Bwawa hili linaweza kutengenezwa na kuweka mahali popote ambapo mfugaji anapohitaji na kulihamisha wakati anapotaka bila kuathiri samaki waliomo ndani yake.

Halikadhalika aina hii ya bwawa ni rahisi kutengeneza na samaki wanakuwa na uhuru Zaidi wa kuzunguka kwa kuwa ni la mviringo.

Ni nini faida za kuwa na aina hii ya bwawa

  • Linaweza kuwekwa mahali popote katika makazi ya mfugaji.
  • Linahamishika kwa urahisi bila kuathiri samaki.
  • Ni rahisi kutengeneza.
  • Samaki wana uhuru Zaidi kwa kuwa ni la mzunguko.
  • Ni rahisi kulihudumia.
  • Usalama wa samaki ni mkubwa.
  • Wakati wote maji yanakuwa na joto linalohitajika kutokana na malighafi zinazotumika kujenga aina hii ya bwawa.
  • Ni rahisi kubadili maji na kuyalekeza kwenye matumizi mengine.
  • Ni rahisi kuvua samaki.
  • Inasaidia kuongeza kipato na kupunguza gharama kwa familia.

Gharama ya kutengeneza bwawa hili ni rahisi sana ukilinganisha na unafuu wa vifaa vinavyohitajika. Gharama inaweza kuwa kati ya shilingi za kitanzania 120,000-400,000/=

Ulishaji

Ulishaji wa vifaranga, chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.

Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food). Hii ni kwa sababu chakula cha  asili amekipata kwenye mbolea iliyowekwa kwenye bwawa. Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Mahitaji ya kutengeneza bwawa rahisi

  • Wiremesh 2 za ukubwa wa futi 7 kwa 4.
  • Blanketi 2 za pamba 4 kwa 6.
  • Turubai futi 25 kwa 20.
  • Karatasi zito la nailoni futi 25 kwa 20.
  • Binding waya kilo 1.
  • Udongo wa kichuguu toroli 2.
  • Mbegu ya samaki kulingana na ukubwa wa bwawa lako.

Kwa maelezo Zaidi unaweza kuwasiliana na Semboja Alvin Semboja kwa simu +255 684 720 400

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

6 maoni juu ya “Ongeza lishe kwa kutumia njia rahisi za ufugaji samaki

    1. Samaki aina ya Kambale wanapofugwa kwenye mabwawa hawana uwezo wa kuzaliana, lakini watazaliana tu endapo wapo kwenye mabwawa makubwa na kuna mzunguko wa maji au maji yanayotembea. Aidha unaweza kuwasiliana na Semboja Alvin Semboja kwa simu +255 684 720 400 kwa maelezo zaidi kama huwa mikoani anatembelea au la! Karibu sana Mkulima Mbunifu

    1. Habari, karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida la MkM. Karatasi hizi zinapatikana kwa wauzaji wa vifaa vya kilimo vya umwagiliaji na makampuni kama vile BALTON Arusha.

      Karibu sana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *