Mifugo wanachangia maisha ya kaya, maisha ya vijijini na uchumi wa nchi. Ni chanzo cha mapato na ajira kwa wazalishaji na wengine wanaofanya kazi katika minyororo ya thamani.
Ufugaji wa mifugo hawa wadogo unahitaji mtaji mdogo kuanzisha, kudumisha, kupanua na wanahitaji eneo ndogo ya kufugia.
Na katika nyakati hizi ambapo kuna mfumuko wa bei ya bidhaa unaosababisha gharama ya maisha kupanda, mifugo wadogo kama kuku, mbuzi, sungura, kondoo na kadhalika ni muhimu hasa katika kutoa lishe mbalimbali kwa kaya, wakiwemo watoto, akina mama na wazee.
Kupata au kumudu vyanzo vya protini kama vile nyama, mayai, samaki, ni changamoto kubwa kwa familia nyingi kwa sababu bei zake ziko juu. Hivyo, mkulima akifuga, mfano, kuku, anaweza kupata mayai yanayotumika nyumbani na hata ya kuuza. Zaidi, mifugo hawa watatoa samadi ambayo ni mbolea nzuri shambani na hutumika kutengeneza mboji.
Maoni kupitia Facebook