- Mifugo

Kuroila: Kuku wa ajabu wenye faida kubwa

Sambaza chapisho hili

Kuroila wanaweza kufugwa ndani na kulishwa katika banda au kuachiwa huru kujitafutia. Wanaweza kulishwa kwa kutumia mabaki ya vyakula au vyakula maalumu.

Kuroila ni aina ya kuku wa kienyeji ambao wanakuwa kwa haraka sana na hutaga mayai mengi zaidi ukilinganisha na aina nyingine ya kuku, wawe wa kienyeji au wa kisasa.

Kwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki, kuku hawa walianza kufugwa nchini Uganda wakitokea India, na sasa wanafugwa pia katika nchi za Kenya na Tanzania.

Nini tofauti yake na kuku wengine

Kuroila wanakuwa kwa haraka sana ukilinganisha na aina nyingine ya kuku wenye asili ya kienyeji. Hawahatamii mayai kama ilivyo kwa kuku wengine wa kienyeji ila hutaga mayai mengi zaidi.

Wakati kuku wa kawaida wa kienyeji anataga mayai 40-50 kwa mwaka, kuroila anataga mayai 200-250 kwa mwaka.

Lishe

Aina hii ya kuku wanaweza kulishwa kwa kutumia vyakula vya kawaida kabisa vinavyopatikana katika mazingira ya mfugaji.

Mfugaji anaweza kulisha aina hii ya kuku kwa kutumia mabaki ya vyakula pamoja na mabaki ya mazao kama vile pumba za mahindi, punje za mahindi na aina za majani yanayopatikana shambani, na bado akapata matokeo sawa na vile ambapo angelisha aina nyingine ya kuku.

Ingawa gharama ya ulishaji wa aina hii ya kuku ni ndogo sana, ni vyema mfugaji akahakikisha kuwa kuku hawa pia wanapata lishe ambayo ni salama kwa afya ya mifugo wake na pia kuweka uhakika zaidi wa ufanisi na usalama wao.

Ni nini faida za kuroila tofauti na kuku wengine

  • Wanakuwa kwa haraka sana
  • Wanastahimili magonjwa ukilinganisha na kuku wengine
  • Wanazalisha mayai kwa wingi sana (200-250)
  • Wanataga kwa muda mrefu zaidi mfululizo (miaka 3)
  • Wana nyama nyingi
  • Mayai yake yana kiini cha njano iliyokolea
  • Wanakula kidogo sana ukilinganisha na aina nyingine ya kuku (kiasi cha gramu 14 tu kwa siku)
  • Wanaweza kufugwa ndani au kuachiwa huru
  • Wanakomaa haraka katika kipindi cha miezi 2-3
  • Wanakuwa na uzito wa kilo 3 hadi 5

Wanazalianaje

Kwa kuwa aina hii ya kuku hutaga mfululizo bila kuhatamia, mfugaji hana budi kutumia kihatamizi kwa ajili ya kuangua vifaranga ili kuendeleza kizazi cha aina hii ya kuku katika shamba lake.

Ni muhimu mfugaji akafahamu namna ya kuchagua mayai yatakayoanguliwa kwa usahihi na kutumia kihatamizi kwa ajili ya kuangua vifaranga watakoendeleza kizazi cha kuroila shambani.

Matunzo ya ziada

Ni muhimu kuhakikisha kuwa kuroila wanapata aina zote za chanjo tangu siku ya kwanza kuanguliwa kama kuku wengine wa kienyeji. Pamoja na kuwa wastahimili magonjwa hii itawasaidia kupambana na mazingira, na kuwa na ufanisi zaidi kwa mfugaji.

Hakikisha unafuata taratibu na hatua zote za chanjo, na endapo una tashwishi juu ya chanjo, tafuta taarifa sahihi au wasiliana na mtaalamu wa mifugo aliyepo karibu na shamba lako.

Kwa maelezo zaidi juu ya uzalishaji na ufugaji wa kuroila, unaweza kuwasiliana na mfugaji, Ombeni Urio kwa simu +255 756641810.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

34 maoni juu ya “Kuroila: Kuku wa ajabu wenye faida kubwa

  1. Habari, nashukuru kwa elemu nzuri ya ufugaji. Nina swali japo litaambatana na maeleo kidogo. Bila shaka twafahamu ya kuwa utengenezaji wa dawa mbalimbali iwe za mifugo au binadamu hutokea katika vyanzo mbalimbali kama mimea,bacteria, fungi na baadhi ya aina za wanyama. Mimi ni mdau katika swala la ufugaji japo ndo kama nimeanza nimepata kufuatilia na kuona baadhi ya mimea ina dawa hitajika za mifugo hususani kuku,pia baadhi ya mimea ni chanjo kwa mifugo kama kuku. Swali LA msingi ni kwamba, je ufugaji wa kuku kwa kutumia njia asili kwa kuwatibu na kuwakinga ni sehemu ya njia bora ya utunzaji wa kuku? na kama sio hivyo ni kwanini?

    1. Habari Tumaini. Karibu sana Mkulima Mbunifu na asante kwa kuwa miongoni mwa wadau na wasomaji wa jarida letu la MkM. Niende moja kwa moja kwenye swali lako, ni sahihi kabisa kuwa ufugaji wa kuku kwa nja ya asili ikihusisha kinga/tiba ni njia bora ya ufugaji wa kuku kwani 1. Ni njia salama ambayo haitumii kemikali za viwandani ambazo ni sumu na amabzo baadaye hupelekea madhara kwa mlaji 2. Ni njia gharama na nafuu kwa mfugaji kwani hutumia malighafi zinazopatikana kwenye eneo lake 3. Ni njia mojawapo yenye tija kwa mfugaji kwani uzalishaji wa kuku na gharama za utunzaji ni ndogo hivyo mfgaji atakapouza kuku wake hupata pato kubwa akishatoa matumizi ya utunzajo. 4. Ni njia inayojali uzalishaji kwa misingi ya kilimo hai

      1. Nashukur kwa makala yako na pole na kajukum swali langu ni je? Kuku hawa naweza kuwapataje

        1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida hili kwa njia ya mtandao. Kuhusu kuwapata kuku hawa, tungefahamu wewe unapatikana mkoa gani ili tuone kama mkoani kwako kuna mtu tunayemfahamu anayejishughulisha na uuzaji.

          Karibu sana

          1. 0759877507, npo mbeya mjini napatane vifaranga wa cku au wk wa kroila na bei yake ni Gani na mnauza kuanzia ndege wangap na ni class gan? Kwa maana F1 au f2 na pia Wana chanjo yote ya awali?

          1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia makala zeti. Kuku hawa wanapatikana inategemea unaishi mkoa gani. Lakini mara nyingi wanauzwa vifaranga na siyo kuku waubwa. Karibu

        1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali toka jarida hili. Kuhusu vifaranga wa kuroila, utawapata kwa wauzaji na wazambazaji wa vifaranga nchini, sisi Mkulima Mbunifu hatuuzi bali tunahusika na kutoa elimu tu. Lakini kama upo Arusha unaweza kuwasiliana na Ombeni Urio kwa simu namba 0756 641 810.

          Karibu Mkulima Mbunifu

  2. mm nipo mkoa wa kilimanjaro wilaya ya mwanga kataq ya jipe nawezaje kuwapata kuku hawa?

    1. Habari, karibu sana Mkulima Mbunifu. Kuna muuzaji anaitwa Ombeni Urio anapatikana Arusha na anasafirisha pia mikoani. Mpigie kwa simu namba 0756 641 810

      Karibu sana

    2. Habari, karibu sana Mkulima Mbunifu. Kuna muuzaji anaitwa Ombeni Urio anapatikana Arusha na anasafirisha pia mikoani. Mpigie kwa simu namba 0756 641 810

  3. Habari pole na majukumu ya Kila siku, naomba kuuliza namna ya usindikaji wa vitunguu swaum ili vikae muda mrefu bila kuharibika nifanyeje

  4. Nashukuru kwa elimu nzuri ya ufugaji wa kuku sasa mmenihamisisha nami nianze kufuga Hawa kuku na ninaamin kuwa endapo nitapata changamoto itakuwa rahis kupata msaada kutoka kwenu

    1. Habari,
      Karibu sana Mkulima Mbunifu na usisiste kuuliza wakati wote tupo kwaajili ya kukuelimisha zaidi

    1. Habari,
      Kuhusu kuku hao huko Zanzibar ngoja tuangalie kama kuna mtu huko anayeuza halafu tutakupa mrejesho

  5. asante sana mkulima mbunifu kwa jarida lako murua, Vipi kwa Dodoma wapi tunaweza kupata msambazaji wa kuiroila?

    1. Habari,

      Kwa Dodoma bado hatuna mtu wa kuamini anayejishughulisha na uuzaji lakini unaweza kuagiza hata toka mikoani na ukatumiwa na ukapata kwa wakati.

  6. Nashukuru sana kwa elimu ya ujasiriamali mnayoitoa. Mimi Niko runzewe Bukombe mkoa wa Geita nawezaje kupata hao vifaranga wa kuku aina ya kuroila.

    1. Habari,

      Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida hili.

      Vifaranga wa kuku wanapataikana kwa wauzaji wa makampuni ya uzalishaji wa vifaranga sehemu mbalimbali nchini, lakini pia unaweza kuwasiliana na Bw.Ombeni Urio toka Arusha kwa simu namba 0756 641 810

      Karibu sana

    1. Habari,

      Karibu sana Mkulima Mbunifu. Inawezekana lakini mpaka tufuatilie kwani kwasasa hatuna mtu tunayemfahamu huko Mbeya anayeuza mayai ya kuku hawa ila kwa Arusha wapo au unaweza kutumiwa vifaranga.

      Karibu sana

        1. Habari,

          Karibu na asante kwa kufuatilia na kusoma makala zetu. Kuhusu wakala hatuna ila unaweza ukanunua kuku kutoka huku Arusha na ukatumiwa.

          Karibu

        2. Habari,

          Karibu na asante kwa kufuatilia na kusoma makala zetu. Kuhusu wakala hatuna ila unaweza ukanunua kuku kutoka huku Arusha na ukatumiwa.

          Karibu

          1. Habari,
            Sisi hatuuzi vifaranga tunatoa elimu tu kwa njia ya machapisho na mitandao ya kijamii. Ili kupata vifaranga ni vyema ukatuambia unapatikana wapi tuweze kukuunganisha na wauzaji wa eneo lako kama tutakuwa nao.

  7. habari, nauliza kuna namna maalum inatakiwa banda la kuku hawa wa kuroiler linatakiwa liwe, baada ya kusoma maelezo yako nimeelewa inabidi nitenganishe ili niweze kupata sehemu nyengine ya kulea vifaranga ili wale wanapokomaa kutaga wengine wawe wameshakuwa na kuanza kutaga.

    1. Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma makala mbalimbali za jarida hili.

      Kwanza banda la kuku aina ya kuroila halina tofauti na banda la kuku wa kienyeji! Ila ni sahihi kuwa kwenye ujenzi wa mabanda ni muhimu kuwa na banda la kuku wakubwa, na banda la kulelea vifaranga. Huwezi kutunza vifaranga na kuku wakubwa katika banda moja au sehemu moja.

      Karibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *