Uchaguzi wa Mbuzi/Kondoo wa Kufuga
Madhumuni ya kuchagua mbuzi au kondoo wa kufuga ni kuboresha uzalishaji na kuendeleza kizazi bora.
Kuna aina nyingi za mbuzi/kondoo wanaoweza kufugwa kulingana na mazingira na mahitaji ya mfugaji.
Uchaguzi hufanyika kwa kuangalia umbile, uzalishaji na kumbukumbu za wazazi kama vile umbo kubwa, ukuaji wa haraka, uwezo wa kutunza vitoto na kutoa maziwa mengi.
Mbuzi/kondoo jike wanaofaa kwa ajili ya kuzalisha maziwa na nyama wawe na sifa zifuatazo;
- Historia ya kukua kwa haraka, kuzaa (ikiwezekana mapacha) na kutunza vitoto vizuri.
- Umbo la mstatili linaloashiria utoaji wa nyama nyingi; na
- Asiwe na ulemavu wa aina yoyote.
Sifa za ziada kwa Mbuzi wa Maziwa
- Awe na miguu ya nyuma iliyo imara na iliyonyooka na yenye nafasi kwa ajili ya kiwele; na
- Awe na kiwele kikubwa na chuchu ndefu zilizokaa vizuri.
Sifa za Dume
Dume bora awe na sifa zifuatazo:-
- Miguu iliyonyooka, imara na yenye nguvu.
- Asiwe na ulemavu wa aina yoyote.
- Mwenye uwezo na nguvu ya kupanda.
- Mwenye kokwa mbili zilizo kaa vizuri na zinazolingana.
Maoni kupitia Facebook