Mkaa wa pumba za mchele hutengenezwa kwa kuchomwa kwa njia maalumu ya kisayansi asilia. Mkaa huchomwa na kuwa na rangi moja ya kikaboni (rangi nyeusi) iliyoiva vyema.
Ndani ya mkaa huu kuna madini ya fosiforasi, potasi, kalshiam, magnesiam, na virutubisho vingi vya asili vinavyohitajika kwa ajili ya kupanda mazao.
Mkaa huu unaweza kutumika kama sehemu mojawapo ya chakula cha nguruwe kwa kuwa kimeunguzwa na kutokuwa na vijidudu pale inapotunzwa vyema.
Pia, hauna vimelea vya magonjwa ya aina yeyote, hivyo haviwezi kumuathiri mnyama.
Matumizi ya mkaa huu
Mkaa huu hutumika kama sehemu ya mbolea ya kioganiki
Hii ni kwa kuchanganya viambatanishi vya kioganiki kama bokashi pamoja na mkaa wa pumba za mchele na inaweza kuwa chanzo kizuri sana cha mbolea ya kioganiki.
Ni kirekebishi cha udongo
Mkaa huu hufanya udongo wa mfinyanzi kutokutuamisha maji na hurudishia virutubisho vilivyo potezwa kwenye mazao muendelezo.
Huweka sawa hali ya ardhi kwa kurudishia mahitaji ya mmea ardhini na kuweka uwezo mkubwa ardhini wa kuwa na unyevu unyevu na kufanya mzunguko wa hewa hitajika katika udongo kuwa mkubwa.
Mkaa huu ni kichanganyio kizuri unapoandaa udongo katika vyungu ukiambatanisha na mbolea pamoja na udongo.
Hutumika kama kabonitaka
Mkaa huu hutumika kuondoa uchafu ulio katika mvunjiko mdogomdogo katika maji na kufanya maji kuwa safi kwa matumizi ya nyumbani au maji ya kunywa.
Hutumika kama kiambatanisho kikuu katika kutengeneza vinyweleo hai
Wakati asilimia 30% hadi 50% ya kabonitaka inapochanganywa na EM bokashi, kwa asili, kabonitaka ni muwezeshaji wa uchocheaji vinyweleo hai ambayo husababisha utengenezaji wa mbolea.
Vinyweleo hai vinaweza kutumika kama kibebeo cha rhizobia naitrojeni inayorekebisha bakteria wanaopatikana katika mizizi ya mikunde.
Ni kidhibiti wadudu
Ina Silica ambayo hufukuza konokono wa dhahabu. Pale inapotumika kwa kuiacha, konokono wanalazimika kutoka nje na kuondoka kwa urahisi.
Ni mkaa wa kupikia
Vijitofali vitengenezwayo kutokana na mkaa wa pumba za mchele ni vizuri sana kama chanzo cha moto. Tofauti na pumba za mchele ambazo hazijageuzwa kuwa kaboni kwani huchukua muda mrefu kuwaka.
Mkaa wa pumba za mchele ni rahisi kuianzishia moto na kuleta moto na hata kubadili joto lake kupikia.
Ni kiondoa harufu au kuzima harufu mbaya (Deodorizer)
Mkaa wa pumba za mchele husaidia kusafisha harufu mbaya ya hewa inayotokana na hewa ya ukaa. Kaboni iliopikwa huyeyusha harufu mbaya hewani vivyo hivyo mkaa huu inapowekwa katika jokofu huweza kuondoa hali ya uvundo.
Mkaa huu hutumika sana katika mabanda ya wanyama kama nguruwe na kuku, kwa ajili ya kupunguza harufu mbaya itokanayo na kinyesi na mkojo wa mifugo.
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na makala hii wasiliana nasi au Mr. Martini Mhando, wa shamba la kilimo hai ST. Joseph Mwanga, Kilimanjaro, kwa simu namba +255 (0)762675234