- Kilimo, Kilimo Biashara

Zingatia afya ya mmea ili kupata mapato mengi

Sambaza chapisho hili

Mara nyingi wakulima wanapuuza maswala yanayohusiana na nafya ya mimea na kupata hasara kubwa. Ikiwa mkulima hatawekeza muda na rasilimali, atakuwa na mimea iliyodhoofika.

Ni nia ya kila mkulima kuwa na mimea yenye nguvu na afya, na yenye uwezo wa kutoa mapato ya hali ya juu. Ni lazima kuwa makini na kuzingatia mbinu zitakazowezesha kufikia lengo hili. Hivyo, swala zima la afya ya mimea huanzia kwenye utayarishaji wa shamba, kurutubisha udongo, kuchagua mbegu na kudhibiti wadudu waharibifu na magonjwa.

Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia ili kuweka mimea kwenye hali ya afya na kuzalisha zaidi.

Tunza udongo ili kutunza mimea

Utunzaji wa udongo unategemeana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya kibiolojia. Kazi kubwa ya baadhi ya viumbe hai waliomo kwenye udongo, ni kumeng’enya mabaki ya mimea na viumbe hai wengine. Mtiririko huu hufanya uwepo wa nguvu, virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa pamoja hutengeneza rutuba kwenye udongo. Utunzaji wa rutuba ya udongo unaongozwa na filosofia hii ‘Lisha udongo ili nao ulishe mimea.’ Udongo wenye rutuba utazalisha mimea yenye afya inayoweza kukabiliana na magonjwa.

Uzalishaji wa mazao kwa njia za asili uhakikisha kunakuwepo uzalishaji wa kutosha bila ya kutumia pembejeo za ziada isipokuwa matandazo, mboji na bila kutifua udongo mara kwa mara. Ongezeko la malighafi za asili husaidia kuimarisha udongo na kufanya kuwepo kwa virutubisho vya kutosha.

Aina ya kilimo cha kisasa na kinachotumia kemikali hufanywa tofauti na ilivyo kwa kilimo hai.

Katika aina hii ya kilimo; udongo hulimwa mara kwa mara jambo linalosababisha uharibifu wa muundo wa udongo, uwiano wa virutubisho, ambapo virutubisho huongezwa kwa kutumia mbolea za viwandani na matandazo hayazingatiwi.

Muundo wa udongo unapobadilika, rutuba nayo hupungua, uwezo wa udongo kuhifadhi maji pamoja na viumbe hai kwenye udongo pia hupungua. Kiwango cha udongo mzuri pia hupungua kwa kuwa hakuna tena viumbe hai wanaotengeneza udongo pia inapunguza mazao kila msimu. Kwa asili mzunguko huu huwa na matokeo yanayoishia kwenye afya ya mimea, na hapa wadudu huchukua nafasi inayowawezesha malengo yao.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *