- Kilimo, Kilimo Biashara

Utengenezaji wa kiuatilifu cha asili

Sambaza chapisho hili

Kama ilivyo ada wakulima wa kilimo hai, huitaji malighafi asili ili kuzalisha mazao salama na yenye ubora shambani.

Si haba, malighafi hizi zinapatikana katika maeneo yetu ya kila siku. Jiulize, Je kwa nini uingie gharama mara mbili ilhali unaweza kutatua changamoto ya wadudu kwa kutumia viuatilifu asili.

Katika makala hii Mkulima Mbunifu inakuangazia, jinsi ya kutengeneza kiuatilifu cha kiasili kinachotokana na mimea mbalimbali.  Mimea hii ina uwezo wa kudhibiti visumbufu vya mimea.

Malighafi

  • Pilipili kichaa (gramu 50)
  • Bangi pori (gramu 50)
  • Sabuni ya maji (Kijiko 1 cha chakula)
  • Muarobaini (Mafuta ya muarobaini vijiko 2 vya chakula)
  • Vitunguu saumu vitatu (3)
  • Lita moja ya maji (1lt)

Jinsi ya kuandaa

  • Katakata majani na maua ya bangi pori, menya vitunguu saumu, katakata pilipili kichaa.
  • Changanya mchanganyiko huo na mafuta ya muarobaini vijiko 2 na sabuni ya maji kijiko 1.
  • Weka maji lita moja alafu koroga ili ichanganyike.
  • Dawa yako itakua tayari kutumika kupulizia katika mazao. Dawa hii inatumika kufukuza wadudu shambani ni anti-bacteria na pia anti-fungus. Inazuia bakteria wabaya na fangasi.

ANGALIZO:

Tengeneza na uitumie papo hapo kwani muda wake kua na nguvu hauzidi siku tatu.

FAHAMU

Jinsi ya kutengeneza mafuta ya muarobaini (Neem oil)

  • Kilo moja (1kg) ya majani ya muarobaini pamoja na mbegu zake
  • Lita moja (1lt) ya mafuta ya nazi au mafuta ya mzeituni
  • Kaanga majani ya muarobaini na mbegu zake ndani ya mafuta ya mzeituni au mafuta ya nazi hadi yatakapo kakamaa na kua rangi nyeusi.
  • Ipua acha ipoe, chuja mafuta yako tayari kwa matumizi.
Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *