- Kilimo, Kilimo Biashara, Mtama, Usindikaji

Unaweza kuongezea thamani Mtama kwa kuzalisha mvinyo

Sambaza chapisho hili

“Kwa karne nyingi, mtama umekuwa ukichukuliwa kama chakula cha watu maskini au chakula cha njaa, hili sasa limegeuka na kutoa matumaini mapya kwa wakulima wa mtama nchini Tanzania”

Mtama ni kundi la mbegu ndogo ndogo aina ya mazao ya nafaka, yanayolimwa sana duniani kote kwa ajili ya chakula na lishe. Hii ni aina ya mazao yanayolimwa katika mazingira magumu kama vile yenye ukame. Mtama umekuwa ukilimwa kwa wingi maeneo ya Asia ya Mashariki, na katika bara la Afrika.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Ni chanzo cha chakula

Mtama ni chanzo kubwa cha chakula katika maeneo yenye ukame na hutumiwa zaidi kama chakula cha kijadi, sehemu mbalimbali duniani na watu wa aina tofauti.

Uji wa mtama hutumika kama chakula cha kijadi cha  warusi na wachina. Halikadhalika, mtama hutumiwa kwa kulisha mifugo hususani ndege.

Nchini Tanzania, mtama hulimwa zaidi katika mikoa ya Singida, Shinyanga, Manyara, Arusha na Kilimanjaro hasa katika wilaya ya Same.

Kilikuwa chakula cha njaa

Kwa miaka kadhaa nchini Tanzania, mtama ulizoeleka kutumiwa kama chakula mbadala wakati wa njaa, na kuzoeleka kama chakula cha watu wenye hali ya chini.

Kutokuna na ukuaji wa elimu na teknolojia ya usindikaji, hivi sasa zao hilo limeweza kupata hadhi na kuzalisha bidhaa kadha wa kadha kwa ajili ya matumizi ya kibinadamu na hata wanyama.

Hali hii inatoa matumaini kwa wakulima wa mtama kwa kuwa sasa wataweza kupata soko la uhakika kwa zao hilo na kujiongezea kipato kutokana na ugunduzi wa namna ya kusindika mtama mwekundu ili kupata mvinyo na bidhaa nyinginezo.

Namna ya kusindika mtama kupata mvinyo

Ili kupata bidhaa iliyo sahihi ni kwa ubora unaotakiwa, ni lazima kuhakikisha kuwa una mahitaji yote yanayotakiwa, pamoja na kuwa na eneo safi na salama lililoandaliwa mahususi kwa ajili ya shughuli za usindikaji.

Ili kupata mvinyo unaotokana na mtama, unahitajika kuwa na:

  • Mtama
  • Sukari
  • Maji
  • Hamira ya mvinyo(wine yeast)
  • Juisi ya tunda lolote isiyoghoshiwa (halisi)

Namna ya kuandaa

  • Chambua mtama vizuri kuondoa takataka
  • Safisha mtama huo vizuri
  • Pasha moto kwa kiwango cha nyuzi joto 30-45
  • Epua na uache kufiki kiwango cha nyuzi joto 15
  • Weka sukari pamoja na hamira kulingana na kiwango unachotaka kutengeneza
  • Changanya na juisi ya tunda ulilochagua kulingana na kiasi unachohitaji kutengeneza
  • Koroga kwa muda wa dakika 5 kila siku kwa muda wa siku 7
  • Baada ya siku 7 chuja kwa kutumia kitambaa safi
  • Baada ya kuchuja weka kwenye dumu linalotoa hewa( Unaweza kuweka mrija kwenye mfuniko) kwa muda wa siku 21
  • Chuja tena kwa kutumia kitambaa safi
  • Weka kwenye dumu lisilopitisha hewa kwa kipindi cha miezi 3.
  • Baada ya muda huo, chuja kwa kitambaa safi tena
  • Weka tena kwenye dumu/chombo kisichopitisha hewa kwa muda wa miezi mingine 3
  • Fungasha tayari kwa matumizi na mauzo

Dondoo

  • Kilo 15 za mtama hutengeneza lita 20 za mvinyo
  • Unahitaji sukari kilo 18 kutengeneza lita 20 za mvinyo
  • Gramu 2.5 za hamira hutumika kutengeneza lita 20 za mvinyo
  • Kutengeneza mchanganyiko huo unahitaji maji lita 20
  • Mchanganyiki huo utahitaji kuwa na juisi lita 1-2

Soko

Mvinyo huo unaweza kuuzwa kwa mtu mmoja mmoja au kwenye maduka makubwa ya vyakula.

Chupa moja ya mvinyo huo yenye ujazo wa mililita 750 inauzwa kwa fedha za kitanzania elfu kumi na mbili (12,000).

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *