Mkulima yeyote atawachukia wadudu kutokana na uharibifu wanaosababisha kwenye mazao. Lakini jambo ambalo wakulima wengi hawalijui ni kuwa kuna baadhi ya wadudu na wanyama ambao ni muhimu sana katika shughuli zao za kilimo. Chukulia mfano wa Fuko ambao huwa wanakula baadhi ya wadudu waharibifu na mashimo yao husaidia kupunguza maji yanayozidi shambani. Ili kupunguza uharibifu wao kwa mimea mkulima anaweza kuweka mafuta ya mbarika kwenye mashimo yao ili kuwasogeza sehemu ambayo hawawezi kusababisha uharibifu kwa mazao.
Maoni kupitia Facebook