Kuna faida nyingi zinazotokana na matumizi ya mbolea za asili kama mboji na nyinginezo. Mbolea asili hutokana na kuoza kwa vitu vyenye uhai kama vile majani, miti na mabaki ya vyakula.
Vitu hivi vinapooza hugeuka na kutengeneza virutubisho ambavyo husaidia kurutubisha udongo na kupunguza gharama kwa mkulima kwa kuwa vitu vinavvyotumika ni vya asili.
Mbolea ya kukuzia mimea inatokana na tope chujio, au mbolea hai inayotokana na kinyesi cha ng’ombe.
Namna ya kutengeneza
Mbolea hii hutengenezwa kwa kuchanganya kinyesi na kiasi cha maji ili mkuweza kunyunyiza kwenye mimea na kutoa matokeo ya haraka kwa muda mfupi.
Mahitaji
Ndoo ya lita 40, kiroba (mfuko), mti, maji, na mbolea hai.
Kutengeneza
- Weka maji robo tatu ya ujazo wa juu kwenye ndoo
- Weka mbolea hai kwenye mfuko ukiwa umeutumbukiza kwenye maji hayo, huku ukiwa umeshikilia kwenye mti uliokatiza juu ya ndoo.
- Funga baada ya maji kujaa kwenye ndoo.
- Acha kwa muda wa siku 3, kisha zungusha taratibu ili kukamua.
- Rudia zoezi hilo kila baada ya siku 3.
- Acha kwa muda wa siku 14, hapo mbolea maji yako itakuwa tayari kwa ajili ya kunyunyizia kwenye mimea yako ili kuikuza.
Matumizi
- Tumia gramu 100 kwa kila mche (unaweza kutumia kikopo cha mafuta kupima).
- Unapoweka mara moja, mboga zitastawi vizuri mpaka wakati wa kuvuna bila kurudia tena.
Mbolea hii ya maji inafaa tu endapo unatumia mbolea ya mboji kwenye shamba lako.
Baada ya siku 14 usitumie tena mbolea hii kwani baada ya hapo itabadilika na kuwa dawa badala ya mbolea