Tumbaku ni dawa ya asili inayoweza kutumika katika kilimo cha mbogamboga
- Tumia ugoro au chemsha miche 20 ya tumbaku.
- Dawa hii inazuia wadudu wanaoshambulia mahindi shambani, wadudu wanaokata miche, kupe, vidukari, viwavi na wengine.
- Chukua gramu 500 za tumbaku, changanya maji lita nane na uchemshe. Chuja baada ya kupoa, ongeza maji lita nane tena na gramu 60 za sabuni ili kuongeza ubora.
- Ni muhimu kuwa na tahadhari kwa kuwa tumbaku ni sumu kwa binadamu na wanyama, hivyo weka mbali na wanyama wafugwao.
Inashauriwa kuvuna mazao siku 4-5 baada ya kunyunyiza aina hii ya dawa.
Maoni kupitia Facebook