- Kilimo

Nimesoma MkM na kupiga hatua katika uzalishaji

Sambaza chapisho hili

Wakulima wengi wamenufaika kutokana na elimu ya bure inayotolewa kupitia jarida hili. Wanasoma na kufanyia majaribio mbinu mbalimbali zinazosimuliwa, uzoefu wa wakulima na watalamu wa kilimo endelevu.

“Tangu mwaka wa 2012, nimekuwa msomaji wa jarida la Mkulima Mbunifu (MkM) na nimepiga hatua kubwa katika uzalishaji”, hivyo ndivyo alivyoanza kujitanabaisha Bw. Godwin Kimaro kutoka Karansi, mkoani Kilimanjaro, alipotembelewa na mwandishi wa jarida hili kwa lengo la kufahamu ni kwa namna gani jarida la Mkulima Mbunifu limekuwa nyenzo katika uzalishaji wa mazao na wanyama kwa wakulima na wanufaika katika eneo hilo.

Bw. Godwin ambaye alionyesha furaha alipotembelewa, alitoa nakala mbalimbali za jarida ambazo amekuwa akipokea kuanzia mwaka 2012. Anasema kwamba amekuwa akizisoma na kuhifadhi, pia akitumia elimu hiyo kwa vitendo katika shughuli zake za uzalishaji. Anaendelea kwamba MkM ni kama darasa kwa wakulima na linajibu changamoto nyingi za wakulima, kwa mfano, kuanzia kuweka malengo ya uzalishaji mpaka kufika kujenga na kudumisha soko.

“Nilianza rasmi kilimo biashara mwaka 2015 huku nikizalisha maharagwe, mahindi, ndizi na mbogamboga. Ingawa kwa uchache, ninafuga ng’ombe, kuku na mbuzi ambao kwa hakika wamekuwa msaada mkubwa kwangu kifedha na kwa chakula kwa familia yangu”, anasimulia.

Kabla ya mafunzo

“Mimi nilikuwa nafanya kilimo, japo kwa kiasi kidogo, lakini nilikuwa nafanya kilimo cha asili yaani natumia mbegu za asili, mbolea za wanyama, hivyo sikuwahi kutumia kabisa mbinu za kisasa kama madawa, mbegu na mbolea katika kuzalisha”, anaeleza.

Anasema kwamba jarida la Mkulima Mbunifu limemsaidia kufahamu na kufanya kilimo ikolojia kwa ukubwa na kupata faida, hasa pale anapozalisha kwa gharama nafuu, kupata mavuno mengi na kufikia soko kwa urahisi.

“Kupitia jarida hili, nimejifunza kufanya kilimo cha matuta ambacho toka awali sikuwa nakifahamu kabisa. Nimejifunza kufanya kilimo cha mbogamboga kwa ukubwa na kwa njia ya kibiashara. Nimeweza kufahamu aina za malisho, namna ya kuzalisha, kulisha mifugo na namna ya kutengeneza na kutumia aina mbalimbali za dawa za asili “, Godwin anaeleza.

“Aidha, nimeweza kujifunza kuhusu ufugaji wa kuku wa asili na kuanza mradi huo. Nimejifunza namna ya kuwapa chanjo kutoka vifaranga wanapoanguliwa mpaka wanapokuwa kuku wakubwa, namna ya kuandaa na kulisha chakula cha kuku, kuweka na kutunza kumbukumbu za uzalishaji”, anaendelea kusimulia.

Bw. Kimaro anasema kuwa yeye pamoja na wanakijiji wengine waliweza kutibu mifugo yao kutokana na ugonjwa wa mapele ngozi mara baada ya kusoma makala kwenye jarida la Septemba 2015, na mpaka sasa wanawachanja mifugo wao kila mwaka na huo ugonjwa haupo tena.

 

Kuhusu wakulima wengine

Wakulima wengi wanawazunguka ni wanufaika wa jarida kwa mara wanapopokea kwenye kikundi chao, wanasoma, kubalishana mawazo, nakala linagusa moja kwa moja shughuli wanazofanya na linatatua changamoto zao hapo kwa hapo.

Changamoto katika kilimo

“Kila penye faida, changamoto hazikosekani na changamoto kubwa ninayokumbana nayo ni ukame, hivyo imenilazimu kuchimba maji ardhini ambayo natumia katika uzalishaji na hunigharimu kuweka umeme kwa ajili ya kupandisha maji na kusambaza shambani”, analalama. Hata hivyo, mkulima huyu anapanda mazao yanyoweza kustahimili ukame ili kuendeleza uzalisha mwaka mzima.

Wito kwa MkM

Bw. Godwin anasema, “Naomba sana wadau wa jarida hili kututembelea mara kwa mara, kwanza kujionea kazi tunazozifanya, lakini pia kushauriana mambo kadhaa yanayotusumbua shambani kwani kuna maswali mengine tunaona tungeweza kupatiwa majibu sahihi ikiwa mtu amejionea mwenyewe kwa macho kile tungependa kuuliza.”

Wito kwa wakulima

“Ningependa kuwashauri wakulima wenzangu kupenda kujisomea jarida hili mara wanapopata, pia kuhifadhi nakala hizi kwa matumizi ya baadaye kwani mimi mpaka sasa nina nakala zangu zote tokea mwaka 2012. Mara kwa mara, narejelea kusoma pale

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *