Wakulima wamekuwa wakipoteza mavuno yatokanayo na mazao kutokana na uvunaji hafifu usiokidhi viwango pamoja na uhifadhi duni.
Ikiwa wakulima wanajiandaa kuelekea kwenye mavuno ni vyema kuhakikisha wanaandaa na kuzingatia kanuni bora za uvunaji ili
waweze kupata mavuno bora na yanayokidhi chakula na soko kwa ujumla.
Wakulima hawana budi kuwa makini na kutambua ni kwa namna gani watavuna mazao yao ikiwa ni pamoja na kuandaa vifaa vya kuvunia kama vile mifuko, vikapu, mikokoteni au matoroli ya kubebea, vifaa vya kukaushia kama vile maturubai, vichanja, pamoja na maeneo na vifaa vya kuhifadhia kama vile magunia, silo, bini, vihenge.