- Kilimo

Mbolea ya BOKASHI inapambana na mbadiliko ya tabianchi

Sambaza chapisho hili

Kutana na mkulima Giranta Giranta, kutoka kijiji cha Bungurere, kata ya Muriba, wilaya ya Tarime, mkoani Mara. Tulizungumza naye kuhusu mbinu za kilimo endelevu anazotumia shambani mwake.

“Najishughulisha na kilimo mseto ambacho imenipa tija kubwa kwenye uzalishaji wa mahindi na maharage. Ninashirikiana na wakulima katika eneo langu na pamoja tumeansiha kikundi kinachijulikana kama Tabukomu”.

Umekumbana na changamoto gani?

Rutuba ya udongo ilikuwa chini na wadudu na magonjwa yalikuwa yanasumbua sana kwenye mazao na kufanya mapato kuwa kidogo.

Mlipata usaidizi gani?

Baada ya kufika mradi wetu wa ASILI B kupitia wawezeshsji wetu wa shirika la TABIO tulipewa mafunzo kuhusu mbinu za kupambana na mabadiliko ya tabia-nchi ikiwemo namna ya kupambana na upoteaji wa rutuba ya udongo, yaani jinsi ya kuongeza rutuba ya udongo ili kuongeza uzalishaji.

Tumejifunza kutengeneza mbolea hai aina ya BOKASHI tukitumia malighafi yafuatayo:

Samadi (mifuko 7) – chanzo cha naitrojeni na vijidudu, Maganda ya mpunga/mahindi (mifuko 7) – kusaidia muundo wa mbolea, Udongo wenye rutuba (mifuko 5) – chanzo cha vijidudu, Unga wa mkaa hai (mfuko 1) – hifadhi ya vijidudu, Pumba (mfuko 1) – chakula cha vijidudu, Molasi (lita 5) – chanzo cha nishati, Hamira (½ kg) – kuchochea uchachushaji, Madini (majivu), na Maji – yasiyo na klorini. Tunachangaya malighafi haya na kupata mbolea mzuri kwa udongo na mimea.

Umepata mafanikio gani?

Kwa sasa nimeweza kuongeza mazoa ya mahindi na maharage kutoka kuvuna gunia 3 ya mahindi na gunia 1 ya maharagwe hadi kufikia magunia 9 ya mahindi na gunia 3 za maharage kwa ekari moja.

Pia, nimepunguza gharama za uzalishaji hasa kununua mbolea za viwandani, badala yake natumia BOKASHI kupandia na kukuzia mimea. Hivyo nimeongea kipato, nina uhakika wa chakula na lishe, nimeongeza bioanuai na kutunza mazingira, na kutoa elimu kwa jamii iliyonizunguka kuhusu ubora na matumizi ya mbolea hii.

Ushauri kwa wakulima Wengine

  • Wakulima watumie mbinu za kilimo mseto na kuachana na kilimo cha mazoea ili kuongeza tija.
  • Tumia mbegu za asili ili kuongeza vyanzo vya virutubisho na kuepuka tatizo la utapia mlo na magonjwa yasiyo yakuambukiza yanayosababishwa na lishe duni.
  • Mbegu za asili zinaweza kupambana na kustahimili athari za mabadiliko ya tabia-nchi.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *