Kudondoka kwa maua kwenye miembe yako inaweza kutokana na upungufu au ukosefu wa aina fulani ya madini.

Virutubisho na madini kwenye miembe vinahitaji ufahamu na uelewa wa hali ya juu kwa kile kinachohitajika. Tofauti na hilo, unahitaji kuzingatia kiasi cha fosiforasi ili kuchochea uwezo wa mizizi na ukuaji wa mmea.
Mkulima anatakiwa kuweka utaratibu wa kuweka mbolea kwenye mimea yake ili kuweza kuboresha virutubisho na rutuba kwa ajili ya mimea yake, na hii itasaidia kuweka uwiano wa ubora na mavuno kutoka katika mazao yake.
Hii inategemea na aina ya udongo katika eneo lako. Ni vyema kwa mkulima kufanya uchambuzi na uchunguzi katika udongo ili kubaini ni aiana ipi ya madini inakosekana.
Kwa wanaofanya kilimo hai, unaweza kutumia njia za asili kama vile kupanda mazao yanayofunika ardhi, matandazo, kutumia mboji na aina nyingine ya matandazo ya asili yanayoweza kuongeza rutuba kwenye udongo. Unashauriwa kutumia mbolea za asili na aina nyinginezo za virutubisho vya asili kila mwaka.
Potashiamu husaidia kuboresha ubora wa maembe, hasa ganda na rangi yake, harufu, ukubwa, na hata uwezo wake wa kukaa muda mrefu. Pia husaidia mmea kustahimili hali ngumu kama vile ukame, baridi, na magonjwa.




