- Kilimo

Kusindika pilipili kali Pilipili husindikwa kupata unga wa pilipili, sosi na lahamu

Sambaza chapisho hili

a) Kusindika pilipili kavu kupata unga

Pilipili kali huumiza macho na pia harufu ikivutwa huleta mkereketo ndani ya pua na kifua wakati wa kusaga ili kupata unga. Inashauriwa kuchukua tahadhari zifuatazo;

Vumbi la pilipili kali huumiza macho hivyo inashauriwa kuvaa miwani ya kukinga macho na vumbi hilo wakati wa kusaga au kufungasha.

Aidha, mtu anayejishughulisha na kazi ya kuchambua, kusaga na kufungasha, anashauriwa kuvaa kinga ya pua kuzuia hewa kali kuingia ndani ya pua na kifuani. Vitu vingine vinavyoshauriwa ni pamoja na uvaaji wa glavu za mikononi, na usafi wa vyombo na mazingira kwa ujumla.

Vifaa
Mashine ya kusaga pilipili, mifuko, na chekeche,

Malighafi
Pilipili kali kavu

Jinsi ya kusindika

  • Chukua pilipili kavu zilizo safi kisha weka kwenye mashine ya kusaga na saga kupata unga
  • Chekecha kwa kutumia chekeche yenye matundu madogo (0.5mm) kisha fungasha kwenye mifuko safi ya nailoni na kisha weka kwenye mifuko ya makaratasi
  • Unga wa pilipili pia unaweza kufungashwa kwenye chupa za kioo zenye mifuniko iliyo na lakiri au karatasi za aluminium au plastiki zinazoshauriwa kuhifadhia chakula
  • Vifungashio kwa ajili ya bidhaa za kuuza viwe na uzito wa gramu 100, 250 na 1000 kulingana na mahitaji ya soko
  • Vifungashio vidogo vidogo vya pilipili viwekwe ndani ya makasha ya mbao au makaratasi magumu
  • Pilipili kavu iliyosagwa inaweza kudumu kwa muda wa mwaka mmoja bila kuharibika ama kupoteza ubora
  • Weka lebo itakayo onesha yafuatayo; Jina la biashara na jina la bidhaa, anuani ya mtengenezaji pamoja na uzito, Tarehe ya kusindika na mwisho wa kutumika kwa bidhaa

Hifadhi mahali safi pakavu na pasipo na mwanga mkali.

Matumizi
Pilipili ya unga iliyosagwa hutumika kama kiungo kwa kuongeza ladha na hamu ya chakula.

b) Kusindika pilipili mbichi kupata sosi (Green Chili Sauce)

Vifaa

  • Mashine ya kusagia rojo na mabeseni ya kuoshea malighafi
  • Bakuli kubwa zitakazotumika kwa ajili ya kuchanganyia rojo
  • Kijiko kikubwa cha chuma cha pua (stainless steel) na mizani
  • Chupa za sosi za plastiki kwa ajili ya kufungashia pamoja na kisu kikali kisichoshika kutu.

Malighafi

  • Pilipili ndefu za kijani kilogramu moja
  • Viazi mviringo gramu 100
  • Chumvi gramu 50
  • Siki miligramu 100
  • Maji safi na salama miligramu 100
  • Tindikali ya sitriki gramu 15
  • Chumvi maalumu aina ya sodium benzoate gramu 72

Jinsi ya kutengeneza

  • Chagua pilipili ndefu zilizokomaa vizuri na ambazo hazikusumbuliwa na wadudu au magonjwa
  • Chambua kuondoa takataka kama majani au matawi na vilevile toa vikonyo kwa mkono na osha kwenye maji safi.
  • Chagua viazi mviringo vilivyokomaa vizuri na menya kuondoa maganda, osha na chemsha hadi viive.
  • Saga pilipili kwa kutumia blenda kisha saga viazi kwa kutumia blenda pia au ponda kwa mwiko hadi viwe laini kabisa.
  • Mimina rojo la pilipili kwenye bakuli kubwa kisha mimina rojo la viazi vilivyopondwa kwenye bakuli hilohilo lenye rojo la pilipili.
  • Changanya vizuri hadi upate uwiano ulio mzuri kisha ongeza gramu 15 za tindikali ya sitriki, gramu 50 za chumvi na gramu 100 za siki
  • Changanya kwenye sosi na koroga vizuri hadi mchanganyiko uwiane.
  • Jaza sosi kwenye chupa za plastiki, funga na mifuniko imara
  • Weka lebo na lakiri kisha hifadhi sehemu safi na yenye mwanga hafifu.

Muhimu
Zingatia usafi wakati wote wa usindikaji ili kupata bidhaa bora na itakayoweza kuhifadhika kwa muda mrefu.
Sosi iliyosindikwa kwa njia hiyo hapo juu huweza kuhifadhika kwa muda wa miezi sita bila kuharibika.

c) Sosi ya pilipili zilizoiva yenye mchanganyiko wa nyanya (Tomato chili sauce)

Vifaa
Jiko, mizani, mashine ya kusaga rojo, chujio, kibao cha kukatia, lebo, kisu kikali kisichoshika kutu, mwiko, sufuria, mabeseni ya kuoshea, kitambaa safi cheupe, refraktomita na kikombe cha kupimia uzito

Malighafi
Nyanya mbivu, sukari, chumvi, siki, wanga wa mahindi, viungo, sodium benzoate, maji safi na salama na unga wa pilipili nyekundu gramu 20 kwa kilo moja ya rojo.

Jinsi ya kutengeneza

  • Chagua nyanya bora zinazotoa rojo nzito kama vile aina za Tanya, Roma au Tengeru 97
  • Osha kwa maji safi na salama kisha ondoa vikonyo na kata vipande vipande
  • Chemsha kwa dakika tatu ili kurahisisha uondoaji wa maganda na mbegu. Ipua na pooza
  • Saga kwa kutumia blenda na chuja kuondoa mbegu na maganda
  • Pima uzito wa rojo kisha ongeza gramu 75 za sukari kwa kilo moja ya rojo
  • Tengeneza mchanganyiko wa viungo ufuatao kwa kila kilo moja ya rojo; pilipili manga gramu 3, mdalasini gramu 3, iliki iliyosagwa gramu 3, karafuu nzima gramu 3, vitunguu maji gramu 50 na pilipili nyekundu ya unga gramu 20
  • Funga viungo vyote kwenye kitambaa safi cheupe na tumbukiza kwenye rojo kisha chemsha ukiwa unakoroga mpaka sosi ifikie nusu ya ujazo wa awali au imekuwa nzito.
  • Ondoa kitambaa chenye viungo kwenye sosi
  • Weka siki gramu 50 kwa kila kilo moja ya rojo ya nyanya kisha ongeza chumvi
  • Changanya wanga wa mahindi gramu 10 kwenye maji kidogo kisha ongeza ndani ya sosi huku ukikoroga • Chemsha kwa dakika tano kisha ipua na weka kwenye chupa za sosi ikiwa na joto lisilopungua nyuzi 70 za sentigredi. Funga kwenye mifuko imara
  • Weka lebo na lakiri kisha hifadhi sehemu yenye ubaridi na mwanga hafifu.

Matumizi ya sosi ya nyanya na pilipili
Sosi hii ya pili na nyanya huliwa pamoja na vyakula mbalimbali il

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *