- Kilimo

Kilimo cha migomba

Sambaza chapisho hili

Musa Hamisi anauliza: Za majukumu Mkulima Mbunifu, naomba kujua ni kipindi gani napaswa kuandaa mashimo na Je, naweza kupanda migomba aina 3 tofauti ndani ya shamba moja lenye ekari moja?

Mkulima Mbunifu: Habari, Karibu Mkulima Mbunifu na asante kwa kuendelea kufuatilia na kusoma machapisho ya MkM.

Migomba huhitaji Kiasi cha chini cha mvua kifaacho ni 100mm kwa mwezi au 1200mm kwa mwaka. Mwinuko ni kutoka usawa wa bahari hadi mita 1800 juu ya usawa wa bahari. Zaidi ya mwinuko huo migomba haikui vizuri.

Kiasi cha joto kinachofaa ni nyuzi joto za sentigredi 25 hadi 30 chini ya nyuzi joto 16 migomba haikui vizuri. Migomba hustawi vizuri kwenye udongo wenye rutuba ya kutosha, kina kirefu, usiotuamisha maji na pia usiwe na chumvi.

Maoni kupitia Facebook
Sambaza chapisho hili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *